Nenda kwa yaliyomo

Wilfrid Napier

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wilfrid Napier

Wilfrid Fox Napier O.F.M. (alizaliwa Matatiele, Afrika Kusini, 8 Machi 1941) ni kiongozi wa kidini kutoka Afrika Kusini katika Kanisa Katoliki. Alitumikia kama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Durban kuanzia mwaka 1992 hadi 2021 na amekuwa kardinali tangu mwaka 2001. Alikuwa Askofu wa Kokstad kuanzia mwaka 1981 hadi 1992.

Napier aliingia katika shirika la Wafransiskani katika kituo cha malezi (novitiate) cha Killarney kabla ya kuhamia Chuo cha Mtakatifu Anthony, Galway, kusoma katika Chuo Kikuu cha Galway (UCG). Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Galway mwaka 1964 na shahada ya Lugha ya Kilatini na Kiingereza. Alisomea pia katika Chuo cha Mtakatifu Anthony cha Wafranciskani cha Ireland huko Leuven, ambako alipata shahada ya uzamili (MA) katika falsafa na theolojia kutoka Chuo Kikuu Katoliki cha Louvain nchini Ubelgiji.[1]

  1. Stober, Paul; Ludman, Barbara (2004). The Mail & Guardian A – Z of South African Politics:The Essential Handbook. South Africa: Jacana Media. ku. 97–8. ISBN 9781770090231.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.