Nenda kwa yaliyomo

Washkaji Wenye Vipaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Washikaji Wenye Vipaji)
Washkaji Wenye Vipaji
Washkaji Wenye Vipaji Cover
Compilation album ya Wasanii Mbalimbali
Imetolewa 2002
Aina Bongo Flava
Lebo MJ Records
Maasai Entertainment ‎
Mtayarishaji Bernard Oduor
Sebastian Maganga


Washkaji Wenye Vipaji ni jina la kutaja albamu ya muziki wa kizazi kipya yenye nyimbo mchanganyiko kutoka kwa wasanii mbalimbali wa Tanzania. Wasanii hao ni pamoja na Da Jo, Bad Spack, Neck Breakerz, Manyema Family, Gangwe Mobb, XPlasterz, Nigger II Public, Jack Warriors, Mr. Shin, Stara Thomas, JC (69) na Q Chief.

Albamu hii ya nyimbo mchanganyiko ulikuwa usimamizi wake Sebastian Maganga na Bernard Oduor. Seba ni miongoni mwa watangazaji waliokuwa wanasimamia kwa jicho la karibu sana uanzishwaji na uendelezi wa muziki wa kizazi kipya kwa mwanzoni mwa miaka ya 2000. Kulikuwa na kipindi kabisa katika Redio Uhuru kuhusu chati za muziki wa kizazi kipya kilichotwa Deiwaka. Kipindi kilikuwa Jumatatu hadi Ijumaa. Kilitumia jina la Deiwaka hadi 2004 kikaitwa Party Up, Hurry Up na muda ukabadilika kutoka saa nane mchana hadi saa kumi, kwenda saa moja usiku hadi saa tatu. Redio pia ilibadilishwa jina kutoka Redio Uhuru hadi Uhuru FM. Kilikuwa kipindi ambacho kilitokea Mkali wa Rhymes.

Kila wiki wanatoka na kuingia wasanii wapya katika chati hizo. Seba pia aliwahi kuwasimamia Gangwe Mobb wakati wa albamu yao ya kwanza "Simulizi la Ufasaha" na hadi kipindi kinaondoka hakuna aliyewahi kupita nafasi za juu katika chati zaidi ya Dully Sykes wimbo wa "Julieta" na Inspector Haroun "Mtoto wa Geti Kali".

Orodha ya nyimbo

[hariri | hariri chanzo]

Orodha ya nyimbo pamoja na watunzi wake. Katika muziki wa Afrika, mara nyingi njia ya usambazaji wa muziki ilikuwa kanda au tepu hivyo jambo la upande A na B ni la kawaida sana.

Upande Jina la Wimbo Jina la msanii
A1 Ulileta Nyodo Da Jo akiwa na Bad Spack
A2 Mlijaribu Hamkuweza Neck Breakerz
A3 Amri Kumi Za Mungu Manyema Family
A4 Heka Heka Gangwe Mobb
A5 Haleluya XPlasterz
B1 Na Bado Nigger II Public
B2 Chuchuchu Jack Warriors
B3 Nakupenda Mr. Shin akiwa Stara
B4 Fani Katika Maisha JC (69) akiwa Q Chief

Kikosi kazi

[hariri | hariri chanzo]

Nyimbo zote zimetayarishwa na MJ Records chini ya watayarishaji mbalimbali wa katika studio hiyo. Upande wa kava la albamu hii ni usanifu wake Thomas Gesthuizen au maarufu kama DJ J4.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]