Nenda kwa yaliyomo

Washeba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maandishi ya Jamii ya Washeba yakiandikwa kwa ajili ya mungu wa mwezi Almaqah
"Mtu wa Shaba" alipatikana katika Al Bayda' (Nashqum ya kale, ufalme wa Sheba), karne ya 6 hadi 5 KK katika makumbusho ya Louvre.
Faili:Sabaean-drachm.jpg

Washeba au Sabæans (Kiarabu: السبأيين‎) walikuwa watu waliokuwa wakizungumza lugha ya Kiarabu cha Kale cha Kusini, waliokuwa wanaishi katika nchi ya sasa Yemen, upande wa Kusini-Magharibi mwa mkono nchi Uarabuni. . Baadhi ya watu wa kabila la Washeba waliwahi kuishi katika eneo la D'mt, lililopo kaskazini mwa Ethiopia na Eritrea, hii ni kutokana na mapenzi yao juu ya Bahari ya Shamu[1].

Historia[hariri | hariri chanzo]

Watu wa kale wa Ufalme wa Sheba' walianza kupotea kufikia katika milenia ya pili hadi kufikia katika karne ya 1 KK. Katika wakati huu, eneo lao lilivamiwa na kukaliwa na watu wa jamii ya Himyar, lakini baada ya kuanguka kwa ufalme wa Himyar uliokuwa ukiongozwa na mfalme Saba na Dhu-Raydan watu wa kabila la Washeba wa kipindi cha kati walitokezea tena. Hii ikiwa ni katika karne ya pili. Lakini hatimaye eneo hili lilivamiwa na kutawaliwa na Himyarite mwishoni mwa karne ya tatu. Mji mkuu wa eneo hili ni Ma'rib. Ufalme huu uliahimia katika pembezoni mwa Jangwa eneo lililoitwa Sayhad na medieval Wanajiografia wa Kiarabu na ndio inayoitwa sasa Ramlat al-Sab`atayn.

Watu wa kabila la Washeba walikuwa ni Waarabu wa Kusini. Na kila kabila katika eneo hili walikuwa na eneo la ufalme wake katika eneo la Yemen ya kale. Jamii ya watu wa Minaeans wakikaa katika eneo la Kaskazini mwa bahari Ya Shamu, na wakati watu wa kabila la Sabeans wakikaa katika upande wa kusini, huku wakiendelea kutanuka kuelekea katika nyanda za juu za bahari.Watu wa jamii ya Qatabanians wakikaa katika upande wa mashariki yao, na jamii ya Hadramites wakikaa upande wao wa Mashariki.

Jamii ya Washeba, kama jamii nyingine yoyote ya Kiarabu na wakazi wa falme za Yemen wa kipindi hicho hicho walikuwa wakijihususha na shughuli za biashara zenye kuleta faida ya hali ya juu. Mara kadhaa walikuwa wakijihusisha na shughuli za Kuuza ubani au uvumba na manemane [2]

Baadhi ya wanahistoria wanaamini kuwa, watu wa jamii zote hizi walikuwa ni watu wa taifa moja wa Ufalme wa Sheba. Waliacha kumbukumbu nyingi katika majengo ya Musnad kama herufi za zamani za Kiarabu, nyaraka kadhaa zilizoandikwa kwa lugha ya Kiarabu.

Nyaraka hizi zilihusu imani ya kuabudu Mungu, na zisijechanganywa na zile za jamii ya Washeba Zilizotajwa katika kitabu kitakatifu cha Quran, ambapo majina yake yameandikwa katika maandishi ya kiarabu pia.

Kutokana na mamalaka yao juu ya Bahari ya Shamu Baadhi ya watu wa kabila la Washeba, walibaki katika eneo la Kaskazini mwa Ethiopiana Eritrea katika kipindi cha Washeba kutaka ufalme wa D`mt. Wanahistoria wengi wanaamini ustaarabu huu kuwa ndio wa asili katika eneo hili,[3] . Lakini wengine bado wanauona kuwa D'mt ni mchanganyiko wa tamaduni kadhaa za makabila mbalimbali yaliyoishi pamoja.;[4] Watu wachache bado wanaendelea kuona Ufalme kuwa wote ni ufalmwe wa Sheba au wa waEritrea na waEthiopia lakini pia wengine husema kuwa, ni wahamiaji wa mwisho wa Sabean lakini ushahidi wao huo wote hua hauna mashiko.

Katika Res Gestae Divi Augusti, Augustus anadai kuwa:

Kwa mamlaka ya utabiri wangu, vikosi viwili vya manajeshi waliongozwa kwa karibu wakati sawa na kuingia katika nchi za Ethiopia na Uarabuni.Nchini Ethipia wavamizi hawa walifika hadi katika mji wa Nabata ulio karibu na mji wa Meroe. Nchini Arabia wanajeshi hawa waliweza kujipenyeza na kufika hadi katika eneo la Mariba[5]

Lakni hata hivyo, maneno haya ya Res Gestae Divi Augusti ni maneno ya propaganda na hakuna sehemu nyingine inayoonesha au kuwa na ushahidi wake.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

 1. Stuart Munro-Hay, Aksum: An African Civilization of Late Antiquity, 1991.
 2. Yemen
 3. Stuart Munro-Hay, Aksum: An African Civilization of Late Antiquity. Edinburgh: University Press, 1991, pp.57.
 4. Taddesse Tamrat, Church and State in Ethiopia: 1270-1527 (Oxford: Oxford University Press, 1972), pp.5-13.
 5. Res Gestae Divi Augusti, paragraph 26.5, translation from Wikisource

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 • Bafaqīh, M. ‛A., L'unification du Yémen antique. La lutte entre Saba’, Himyar et le Hadramawt de Ier au IIIème siècle de l'ère chrétienne. Paris, 1990 (Bibliothèque de Raydan, 1).
 • Andrey Korotayev. Ancient Yemen. Oxford: Oxford University Press, 1995. ISBN 0-19-922237-1[1].
 • Andrey Korotayev. Pre-Islamic Yemen. Wiesbaden: Harrassowitz Verlag, 1996. ISBN 3-447-03679-6.
 • Ryckmans, J., Müller, W. W., and ‛Abdallah, Yu., Textes du Yémen Antique inscrits sur bois. Louvain-la-Neuve, 1994 (Publications de l'Institut Orientaliste de Louvain, 43).
 • Info Please
 • Article at Encyclopedia Britannica

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]