Majadiliano:Washeba
Jina??
[hariri chanzo]Naona chaguo la jina liangaliwe upya. Si vema kutumia umbo la Kiingereza la umbo la Kigiriki/Kilatini la jina la watu hawa. Maana habari za watu hao zinapatikana katika Biblia kwa jina la "watu wa Sheba" (Yoeli 3,8) , "Majeshi ya Sheba" (Ayubu 6.19), na mahali pengi pengine. Kwa hiyo jina la nchi kwa Kiswahili ni "Sheba".
Pia kuna bado matatizo ya tahajia pamoja na lugha kwa jumla (ling. viungo vyekundu kama "Mkono nchi wa Arabian" (??), "Old South Arabian" (???), "Red Sea" (makala yake iko kwa jina la Kiswahili!), "karne ya kwanza kabla ya Kifo cha Kristu" (hesabu ya karne kabla ya KIFO??)
Pamoja na hayo kwa bahati mbaya kuna sentensi zinazofuata muundo wa Kiingereza kwa maneno ya Kiswahili jambo lisiloweza kufurahisha wala kueleweka "Watu wachache wbado wanaendelea kuona Ufalme kuwa wote ni ufalmww wa Sabaean au wa waEritrea na waEthiopia lakini pia wengine husema kuwa. ni wahamiaji wa mwisho wa Sabean lakini wote hutoa ushahidi ambao hauna nguvu." --Kipala (majadiliano) 10:35, 15 Januari 2010 (UTC)