Nenda kwa yaliyomo

Waseri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Waseri ni kabila la watu linalopatikana kwa wingi kaskazini mwa Mkoa wa Kilimanjaro, ambao lugha yao ni Kiseri.

Waseri wanajishugulisha sana kwa kilimo, ufugaji, biashara na kazi za ofisini. Pia wanaweza kufanya kazi zingine za ufundi n.k. Waseri wanapatikana hususani kuanzia maeneo ya Kirongo, Tarakea, Rongai na Holili.

Lugha ya kiseri ni miongoni mwa Lugha za Kibantu zilizoainishwa na Malcolm Guthrie. [1]

  1. Guthrie, Malcolm (2017-09-22), "II Identifying the Bantu Languages", The Classification of the Bantu Languages bound with Bantu Word Division, Routledge, ku. 6–13, ISBN 978-1-315-10553-6, iliwekwa mnamo 2023-10-13