Walter Mongare Nyambane
Walter "Nyambane" Mongare (aliyezaliwa 1975) ni mwanasarakasi, mwigizaji na mwimbaji wa nyimbo za maskharani mzaliwa wa Kenya. Amekuwa maarufu katika sarakasi ya kaya ijulikanayo kama Reddykyulass . Yeye ni maarufu sana kwa kuigiza kama Rais wa Kenya Daniel Arap Moi katika Reddykyulass.
Elimu[hariri | hariri chanzo]
Walter alihudhuria Shule ya upili ya Lenana, kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Redio[hariri | hariri chanzo]
Amewahi kufanya kazi na shirika la utangazaji la Kiss 100 kama mtangazaji wa kipindi cha asubuhi The Big Breakfast huku akishirikiana na mtangazaji mwenzake Caroline Mutuku. Hatimaye alitoka huko[1] na kwenda kufanya kazi ya utangazaji katika kituo cha Q Fm ambacho kinamilikiwa na Kampuni ya Utangazaji ya Nation Media Group.
Runinga[hariri | hariri chanzo]
Ameigiza katika Sarakasi ya Redykyulass , msimu wa 1-4.
Pia ameigiza katika Red KORNA , msimu wa 1 na 2.
Licha ya hayo, Walter hujishughulisha na matangazo ya Biashara katika Runinga pia.
Nyimbo Zake[hariri | hariri chanzo]
Sweet Banana akimshirikisha Talia
Must be Nyambane akimshirikisha Natasha Gatabaki
Slowly my Dear akimshirikisha Sanaipei Tande / Megcy
Dereva wawili akishirikiana na Prince Adio
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]
Video[hariri | hariri chanzo]
- Majadiliano kati ya Citizen Tv na Walter Mongare kwa hisani ya Youtube