Nenda kwa yaliyomo

Waconzy

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Waconzy

Obinna Kelvin Anyanwu (anajulikana zaidi kwa jina la kisanii Waconzy; amezaliwa Port Harcourt, Rivers State, 10 Agosti 1983) ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa muziki, mfanyabiashara na mfadhili, mwenye asili ya kifamilia kutoka Umuahia, mji mkuu wa Abia State, kusini mashariki mwa Nigeria. Pia ndiye mwanzilishi wa Dv8 Media na Waconzy Foundation. Alipata umaarufu mwaka 2010 kupitia wimbo wake "I Celebrate" uliokuwa kwenye albamu yake ya I Celebrate. Albamu yake ya pili Money Back Guarantee ilitolewa mwaka 2013. Hivi sasa amesajiliwa chini ya lebo ya Dv8 Media.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Waconzy alizaliwa Port Harcourt, mji mkuu wa Rivers State, kusini mwa Nigeria na alimaliza elimu yake ya msingi na sekondari huko. Mwaka 1998, akiwa bado katika shule ya sekondari, alirekodi wimbo wake wa kwanza.[1]

Mwaka 2000, alipata nafasi ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Shirikisho Owerri na alihitimu mwaka 2005 na shahada ya Bachelor of Technology katika usimamizi wa miradi. Baada ya kukamilisha program yake ya NYSC mwaka 2006, Waconzy alijiunga na chuo cha Project Management Institute nchini Marekani ambapo alipata cheti cha Project Management Professional (PMP). Kisha, mwaka 2008, alianzisha kampuni yake ya Dv8 Media.[2][3]

  1. "Early life Story of Waconzy". Jango.
  2. "Early life Story of Waconzy". Waconzy. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-11-25.
  3. "Waconzy 'buys over Dv8 media with $100,000". The Net. {{cite web}}: line feed character in |publisher= at position 4 (help)
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waconzy kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.