Vladimir Vuletić
| Vladimir Vuletić | |
|---|---|
| | |
| Alizaliwa | 28 Novemba 1978 |
| Wazazi | wakili wa Serbia |
Vladimir Vuletić (alizaliwa 28 Novemba 1978) ni wakili wa Serbia, profesa msaidizi katika Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Belgrade na makamu wa rais wa zamani wa FK Partizan.
Maisha ya Awali na Elimu
[hariri | hariri chanzo]Vladimir Alizaliwa tarehe 28 Novemba 1978 huko Šabac, wakati huo sehemu ya SR Serbia na SFR Yugoslavia. mbapo alimaliza shule ya msingi "Janko Veselinović" na kisha Šabac Gymnasium.[1]
Kazi Katika Taaluma
[hariri | hariri chanzo]Vladimir Alichaguliwa kuwa mkufunzi msaidizi katika Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Belgrade katika uwanja wa sheria ya Kirumi mnamo Machi 2003. Akawa msaidizi mnamo Juni 2007.
Aliteuliwa kuwa profesa msaidizi mnamo Machi 2011. Alikuwa Katibu wa Idara ya Historia ya Sheria kuanzia mwaka 2003 hadi 2008. Kwa sasa ni profesa mshiriki katika Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Belgrade.
FK Partizan
[hariri | hariri chanzo]Katika mkutano mkuu wa mwaka wa FK Partizan, mwezi Desemba 2014, alichaguliwa kuwa rais wa Bodi ya Usimamizi ya klabu hiyo.[2]
Vuletić alihudumu kama makamu wa rais wa FK Partizan hadi alipowasilisha kujiuzulu tarehe 9 Februari 2021, kufuatia kukamatwa kwa wanachama wa kundi la mashabiki wa FK Partizan Grobari, na kugunduliwa kwa mabohari yaliyokuwa yamefichwa katika Uwanja wa Partizan ambayo yalitumika kwa shughuli za kihalifu.[3][4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "UZ NOVOG PREDSEDNIKA: Ko čini novi Upravni odbor FK Partizan!? - Domaći fudbal, Fudbal". HotSport (kwa Kiserbia). Iliwekwa mnamo 2014-12-25.
- ↑ "UZ NOVOG PREDSEDNIKA: Ko čini novi Upravni odbor FK Partizan!? - Domaći fudbal, Fudbal". HotSport (kwa Kiserbia). 2014-12-25. Iliwekwa mnamo 2021-03-09.
- ↑ Vojvodine, Javna medijska ustanova JMU Radio-televizija. "Potpredsednik FK Partizan Vladimir Vuletić podneo ostavku". JMU Radio-televizija Vojvodine. Iliwekwa mnamo 2021-03-09.
- ↑ "Vuletić podneo ostavku na mesto potpredsednika FK Partizan - Sport - Dnevni list Danas". www.danas.rs (kwa Kiserbia). Iliwekwa mnamo 2021-03-09.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Vladimir Vuletić kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |