Nenda kwa yaliyomo

Visasili vya Kimasai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Visasili vya Kimasai ni imani za jadi za Wamasai wa Kenya na Tanzania. Katika utamaduni wao, asili na mambo yake ni sura muhimu za dini zao.[1]

Ngai (pia huitwa Engai au Enkai, yaani "mvua." [2]) ndiye Muumba Mkuu ambae muonekano wake kwa sehemu moja ni wa kike na wa kiume, anayemiliki kanuni za kiume na za kike.[3] Wamasai hurejelea makao ya awali ya Ngai kama "Ol Doinyo Lengai" ambayo maana yake halisi ni "Mlima wa Mungu", ambayo wanaamini iko Kaskazini mwa Tanzania.[3]

Katika dini ya Kimaasai, Laibon (wingi: Laiboni) huingilia kati ya ulimwengu wa walio hai na Muumba. Hao ndio makuhani wakuu na waaguzi wa Wamasai. Zaidi ya kupanga na kusimamia sherehe za kidini ikihusisha dhabihu na matoleo, wao pia huponya walio hai, kimwili na kiroho.[4]

  1. "Bron Taylor", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2023-03-30, iliwekwa mnamo 2023-05-14
  2. "Sigurd Bergmann", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2023-01-12, iliwekwa mnamo 2023-05-14
  3. 3.0 3.1 "Molefi Kete Asante", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2023-05-08, iliwekwa mnamo 2023-05-14
  4. Asante, Molefi Kete; Mazama, Ama; Encyclopedia of African Religion, Volume 1, SAGE (2009), [p. 428, ISBN 9781412936361 (retrieved March 18, 2020)
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Visasili vya Kimasai kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.