Nenda kwa yaliyomo

Vijana wa Algeria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Vijana wa Algeria (Kifaransa: Jeunes Algériens) walikuwa kundi la kisiasa lililoanzishwa katika kipindi cha Algeria ya Kifaransa mnamo mwaka mwaka 1907. Walikuwa wafuasi wa mtazamo wa kuunganisha, maana yake walitaka jamii ya Algeria kuungana na jamii ya kikoloni ya Kifaransa. Kwa hivyo, walidai mageuzi ambayo yangewapa raia wa Algeria haki sawa na zile zilizofurahiwa na raia wa Ufaransa.

Watu mashuhuri katika kundi hili walijumuisha Khalid ibn Hashim na Ferhat Abbas.[1]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Lawrence, Adria K. (2013). Imperial Rule and the Politics of Nationalism: Anti-Colonial Protest in the French Empire. Cambridge University Press. ku. 74–78, 84–85. ISBN 978-1-107-03709-0.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vijana wa Algeria kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.