Victoria Kisyombe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Victoria Kisyombe (alizaliwa tar.) ni mwanzilishi wa kampuni ya SELFINA iliyopo nchini Tanzania inayohusika na utoaji mikopo midogo kwa wanawake, hasa wajane, kwa lengo la kuwawezesha kujikwamua katika dimbwi la umaskini na utegemezi nchini.

Kwa malengo na ubunifu wake, amefanikiwa kusaidia wanawake 27,000 na kutengeneza nafasi 150,000 za ajira.[1]

Elimu yake[hariri | hariri chanzo]

Alipata elimu yake ya msingi na sekondari mkoani Mbeya kabla ya kuhamia nchini Kenya kumalizia mafunzo yake.

Alirejea nchini Tanzania na kupata shahada ya sayansi ya mifugo mwaka 1983.

Mwaka 1986 alipata ufadhili kutoka chuo kukuu cha Edinburgh na kupata shahada ya udhamili.[2]

Kazi yake[hariri | hariri chanzo]

Ni mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya SELFINA tangu mwaka 2002.

Tuzo zake[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2009 alipata tuzo ya TIAW tofauti ya dunia ya 100 kwa kutambua mchango wake bora katika kufanya tofauti duniani.[3]

Mwaka 2010 alipata tuzo ya mjasiriamali bora wa kijamii Afrika.

Mwaka 2014 alipata tuzo ya uongozi wa kimataifa juu ya uwezeshaji wa kiuchumi.

Mwaka 2016 alipata tuzo ya Mwanamke wa Afrika wa mwaka katika biashara, fedha na benki.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]