Nenda kwa yaliyomo

Toi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Vichezeo)
Makala hii kuhusu "Toi" inatumia neno au maneno ambayo si ya kawaida; matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

Gololi (hapa za kioo) ni vichezeo vinavyopendwa kote duniani

Toi[1] (ing. toy), pia kichezeo[2] ni kitu cha kuchezea, hasa kwa watoto.

Mifano yake ni mwanasesere, mpira au gololi. Lakini si watoto pekee wanaotumia toi hutumiwa pia na watu wazima au wanyama. Kwa mfano paka hupenda kucheza kwa mpira.

Katika mazingira ya kijadi watoto wanatumia vitu vinavyopatikana kiasili kama mawe na mafimbo. Halafu wanatumia udongo wa kushikana (kama udongo wa mfinyazi) na kufinyanga vidoli.

Mahali pengi wazazi waliwatengenezea watoto toi za aina mbalimbali. Watoto walipewa pia au kujitengenezea vifaa vidogo vya kufanana na vifaa vya wtu wazima. Mifano ni pinde na mishale midogo, au sufuria za kuiga shughuli za wakubwa.

Katika mazingira ya mjini watu walianza kutengeneza toi na kuziuza.

Katika utamaduni wa Ugiriki ya Kale ilikuwa kawaida ya kwamba watoto walitoa vichezeo kama sadaka kwa miungu kwenye hekalu wakati wa kubalehe kama ishara ya kwamba wamekuwa wakubwa sasa.[3]

Katika mazingira ya kisasa toi zimekuwa biashara kubwa. Hutengenezwa viwandani na kupelekwa kote duniani. Kwa mfano huko Marekani biashara ya vitu vya kuchezea ilikuwa na thamani ya bilioni 22.9 za dolar za Marekani. Asilimia 88 za biashara hii ilikuwa kwa watoto wenye umri wa miaka 0–11. Asilimia 75% za vichezeo vyote vilivyouzwa Marekani vilitengenezwa huko China. [4]

Picha za toi

[hariri | hariri chanzo]
  1. "toi" ni jaribio la kutumia neno la Kiingereza jinsi linavyoweza kusikika mjini Dar es Salaam kwa jambo ingawa haionekani katika maandishi ya Kiswahili,
  2. Kichezeo si neno la kawaida kwa Kiswahili; hadi sasa hakuna nomino moja kwa "kitu cha kuchezea" lililo kawaida kwa Kiswahili. "Kichezeo" imewahi kutumiwa mara chache kwenye blogu kadhaa na kurasa nyingine. Inapatikana pia katika kamusi ya Legere, Kijerumani-Kiswahili
  3. Powell, Barry B. (2001). Classical Myth; Third Edition. Upper Saddle River, NJ: Prentice Hall. pp. 33–34. ISBN 0-13-088442-1 .
  4. "Data za kisasa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-05-07. Iliwekwa mnamo 2015-05-19.