Nenda kwa yaliyomo

Viatu vya Faith

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Viatu vya Faith
Jina la kampuni Viatu vya Faith
Ilianzishwa 1964
Mwanzilishi Samuel Faith
Aina ya kampuni Biashara ya familia
Bidhaa zinazosambazwa na kampuni hii Viatu
Nchi Uingereza
Tovuti http://www.faith.co.uk/

Viatu vya Faith ni kampuni ya kuunda viatu ya Uingereza ambayo ilianzishwa katika mwaka wa 1964 na mhasibu wa London aliyeitwa Samuel Faith na mke wake,Terri. Baada ya Samuel kustaafu, mwanawe Jonathan alichukua usimamizi wa biashara hiyo,ya familia.

Katika miaka ya 1980, kampuni ilianzisha aina mpya ya viatu iliyofanikiwa sana ilitoitwa "faith solo", ikichukua mitindo mipya iliyoundwa katika maonyesho ya washonaji na kuunda viatu vya kuvaliwa na raia wa kawaida.

Aina hiyo ya viatu ilisherehekea mwaka wake wa 40 ,katika mwaka wa 2004, na ina matawi 70 yanayojisimamia yenyewe.Vilevile,kampuni hii ina maduka ndani ya Allders, Debenhams ,Sunwin House na Beatties. Hapo Desemba 2004, kampuni ya Viatu vya Faith ilinunuliwa na kundi la kibinafsi la Bridgepoint Capital.

Hivi sasa kuna duka moja tu la Faith ndani ya Topshop (katika Oxford Circus). Topshop iliagiza Faith kuondoka katika maduka yake katika majira ya joto ya 2003, ilipoona kuwa watapata faida zaidi wakijiundia viatu vyao vyenyewe na kuviuza. Hata hivyo,hii ilisababisha upanuzi wa matawi ya Faith na ,hivyo basi, kuiongezea faida.

Mauzo na Umiliki

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kuuzwa kwa Faith, Jacqueline O'Neill alichukua nafasi ya mkurugenzi kuu kabla ya kustaafu katika mwaka wa 2007. Paul O'Neill,mume wake, alikuwa kwenye bodi ya wakurugenzi na alishughulika na mali; akaongoza Faith kushinda tuzo nyingi za Retail Award. Aliondoka katika mwaka wa 2008 ili kuzingatia malengo yake mengine.

  1. Viatu vya Faith Archived 27 Januari 2010 at the Wayback Machine.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]