Nenda kwa yaliyomo

VICOBA

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

VICOBA ni kifupi cha maneno ya Kiingereza yakiwa na maana ya “Village Community Banks”. Neno VICOBA lilibuniwa na Salim Zagar wakati akiwa mtumishi wa shirika la dini na amani ulimwenguni, tawi la Tanzania (World Conference on Religions for Peace/Tanzania) WCRP/Tz.

VICOBA ni mikopo midogo midogo ambayo imekuwa ikitolewa kwa kaya maskini na za kipato cha chini kwa ajili ya biashara zao ndogondogo na wafanyabiashara wadogo ili kuwawezesha kuinua viwango vyao vya mapato na kuboresha hali zao za maisha. Mikopo hii imewahakikisha wanawake kujitegemea kupitia kufanya na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi na imekuwa inakuza ujumuishaji wa watu maskini katika mchakato wa ukuaji wa uchumi, watu ambao hawana fursa ya soko rasmi la ajira mara nyingi wamekuwa wakifaidika kwa kuunganisha rasilimali na kufanya kazi katika vikundi hivyo.

Mfumo wa VICOBA umetokana na uboreshaji wa mfumo wa “Mata Masu Dubala” (MMD) ulioanzishwa nchini Niger mwaka 1991 na shirika la Care International.[1]

VICOBA vimekuwa mkombozi wa maisha kwa watu wengi hususani wanawake na vijana kutokana na kwamba wamekuwa wakiendesha shughuli zao wenyewe na kujipatia kipato ambacho kimekuwa kikiwasaidia kuepukana dhidi ya vitendo vya ukatili, unyanyasaji na mateso kutoka katika makundi mbalimbali ikiwemo mifumo dume. [2]

Katika utafiti mbalimbali, inaonesha kuwa baadhi ya wanawake wamebadilisha maisha yao kutoka maisha duni hadi maisha bora kutokana na VICOBA.

Kwa mujibu wa Louise Pizon, mwandishi wa makala kuhusiana na VICOBA kutoka Shule ya Biashara ya ESSEC, Master in Strategy & Management of International Business (SMIB), (2020-2022) miongoni mwa wanufaika wa mikopo hiyo ni pamoja na Mary Charles ambaye ni mfanyabiashara. [3]

Utafiti unaonesha kuwa wanufaika wa mikopo wamebadilisha maisha yao kwa kiwango kikubwa hususani wanawake na inatajwa kuwa idadi kubwa ya wanufakao wa mikopo hiyo ni wanawake kuliko ilivyo kwa wanaume[4].

Kwa mujibu wa utafiti wa Mwaka 2014, wa kutathmini athari za mpango wa VICOBA katika kipindi cha miaka minne, idadi ya wanufaika wa VICOBA imeongezeka mara nne tangu mwaka 2011, jumla ya watu ambao wamefaidika na mpango huo ni 294, idadi ya wanaume wanaojiunga na mpango huo imeongezeka kutoka asilimia 4 mwaka 2011 hadi asilimia 12 mwaka 2014, wanawake waliendelea kuongoza katika kushawishi maendeleo ya jamii kupitia mikopo ya VICOBA, kati ya wanaojihusisha na mpango wa VICOBA, asilimia 10 ni wazazi au walezi wa watoto wenye ulemavu, ambapo familia hizo zinawezeshwa kupambana na umaskini, halikadhalika kwa upande wa ufadhili, asilimia 51 ya washiriki waliokopa kutoka benki ya jamii ya VICOBA, walitumia fedha hizo kuanzisha biashara zao na kutengeneza fursa za kujiajiri. [5]

Biashara ambazo zimekuwa zikianzishwa kwa kukopa VICOBA ni pamoja na: Ufugaji (Nguruwe, Kuku na Ng'ombe), mazao, maduka ya reja reja, mabanda ya bustani ya mboga mboga, biashara za ushonaji nguo, migahawa, na ujenzi wa nyumba za kupangisha. Takriban asilimia 90 ya wakopaji wa VICOBA wanajihusisha na kilimo. Mpango wa VICOBA umesababisha kuimarika kwa mapato ya kaya ya washiriki jambo ambalo limesaidia familia kukidhi mahitaji yao ya kimsingi kama vile chakula, malazi na elimu na kupunguza ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake katika jamii. [6]

Aidha kwa mujibu wa utafiti wa Joseph Magali. (2021), uliolenga kuangazia Wajibu wa Benki za Jumuiya ya Kijiji (VICOBA) Mikopo Midogo katika Kukuza Uendelezaji wa Viwanda Vidogo na Vidogo Endelevu katika Mkoa wa Kilimanjaro, ukuaji wa viwanda endelevu unahusishwa na maisha endelevu ya wateja wa VICOBA ambapo Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa mikopo midogo midogo ya VICOBA imetekeleza majukumu mbalimbali katika kukuza uchumi endelevu wa viwanda vidogo mkoani Kilimanjaro ambapo imesaidia uzalishaji wa malighafi, kuwa chanzo cha ujasiriamali wa viwanda na kuwezesha mafunzo katika masuala ya uanzishaji viwanda. Pia, utafiti huo umebaini kuwa changamoto zinazokabili viwanda vidogo vinavyomilikiwa na wanachama wa VICOBA ni uzalishaji mdogo, masoko ya uhakika ya bidhaa, imani ndogo kwa jamii na mitaji duni. [7] [8]

Hata hivyo Shirika la World Wildlife Fund for Nature (WWF) Tanzania, katika taarifa zake limebainisha kuwa VICOBA vimekuwa msaada mkubwa kwa akina mama wa vijijini kuondokana na mila na desturi kandamizi hususani za kukosa usawa wa kiuchumi katika jamii, ambapo katika taarifa yake, Jinsi benki za kijamii zinavyowawezesha wanawake nchini Tanzania, limeeleza kuwa changamoto kama Wanawake kuwa na mwelekeo mdogo wa kupata umiliki wa mali, mikopo, mafunzo na ajira kuliko wanaume, umezidi kupungua kutokana na wanawake kujihusisha na biashara mbalimbali baada ya kupata mikopo ya VICOBA. [9][10][11]

Historia ya mfumo wa VICOBA

[hariri | hariri chanzo]

Mfumo wa VICOBA unalenga kusaidia jamii zinazoishi katika hali ya umaskini na zenye kipato cha chini ili ziweze kujikwamua na umaskini hasa katika ngazi ya familia. VICOBA ni daraja la kusaidia washiriki kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kimazingira.

Hii imewezekana kwa utaratibu wa kutoa mafunzo kwa wanakikundi kuhusu kazi za mikono na shughuli nyengine ndogo ndogo za kiuchumi (MSMEs) ambazo zinaongeza kipato cha familia. Mfumo huu unaweka mkazo katika umiliki wa jamii ambapo wanakikundi wanakuwa ndio wamiliki wa mali yote ya kikundi, ikilinganishwa na mifumo mingine ya ukopeshaji fedha, kwa mfano benki, mkopeshaji ndiye anayemiliki mali na mkopaji anakuwa ni chombo tu cha kumzalishia faida.

Mfumo wa MMD uliingia Tanzania mwaka 2000 na ulianza kutekelezwa Tanzania Visiwani (Zanzibar) kupitia mradi ulioanzishwa na shirika la CARE International katika eneo la mji wa Jozani. Mradi huu ulifahamika kama Jozani Savings and Credit Association (JOSACA).

Baada ya hapo shirika la WCRP tawi la Tanzania lilijifunza namna mfumo huu unavyofanya kazi na kisha kuuleta Tanzania Bara mwaka 2002 kwa ushirikiano na Bwana George Swevetta aliyekuwa mfanyakazi wa CARE International kule Jozani. Mpango wa MMD ulianzishwa kwa majaribio katika Kata ya Ukonga, Wilaya ya Ilala, mkoa wa Dar es Salaam na wilaya ya Kisarawe, mkoa wa Pwani. [12]

Majaribio hayo yalilenga kuondoa udhaifu uliojitokeza kwenye mradi wa Jozani ili kukidhi mazingira ya Tanzania Bara. Maboresho yaliyofanyika yalizaa mfumo wa VICOBA ambao unaendana na mila na desturi za Tanzania Bara. Maendeleo makubwa katika mfumo wa VICOBA yamevutia wadau mbalimbali ikiwemo Serikali na wahisani. Serikali kupitia Kitengo cha Kupunguza Umaskini Tanzania kilichokuwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais mwanzoni mwa miaka ya 2000 kilivutiwa na mfumo wa VICOBA kama moja ya nyenzo ya kupambana na umaskini na kiliweka azimio la kuandaa mpango wa Kitaifa wa kueneza VICOBA Tanzania. Kitengo hiki ambacho kwa sasa kiko chini ya Wizara ya Fedha na Mipango (MoFP) kimekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha mfumo huu kutumika maeneo ya vijijini na hata mijini.

Kitengo hicho kilishirikiana na shirika la Social and Econmic Development Initiatives of Tanzania (SEDIT) kuanzisha miradi ya kueneza mfumo wa VICOBA katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara, Lindi, Kilimanjaro. Baadae mfumo huo uliendelea kuenezwa na wadau wengine kama vile World Wide Fund for Nature/Tanzania (WWF/Tz), National Income Generation Programme (NIGP), Land Management Programme (LAMP), ORGUT, FRANKFRUIT ZOOLOGY, VETAID, KKKT, SONGAS, LIMAS, Plan Internationalna, Norwegian Church Aid (NCA). [13]

VICOBA huundwa na wanachama kati ya 15 hadi 30 ambao wamejichagua wenyewe, huku pia Wanachama huanza kununua hisa kwenye kikundi na baada ya wiki kumi na mbili mfuko wa hisa huanza kukopeshwa kwa wanachama wake. Uanachama wa vikundi vya VICOBA uko wazi kwa wanawake na wanaume na angalau wajumbe wawili kati ya watano wa kamati ya uongozi lazima wawe wanawake. [14]

Baadhi ya wadau wa VICOBA nchini ambao kwa miaka mingi sasa wamekuwa wanahamashisha vikundi katika maeneo mbalimbali ni pamoja na IRCPT, UPEO, TEC, CCT, BAKWATA, AEE, Pathfinder International, AFRICARE, LAMP, LIWODET, MEPP, RUMAKI, Social EconomicDevelopment Initiative of Tanzania, SELL, VDSA, WWF, ORGUT, FLORESTA, ELCT(ND, ECD,Mbulu) TCRS, TANARELA, AXIOUS Foundation, WCST, ITECCO, Frankfurt Zoological Society, UYACODE, YWCA, EFG na wengine wengi. Maeneo mbalimbali ya Tanzaniayameweza kufikiwa japo siyo wadau wote wanatekeleza mfumo huu kama inavyotakiwa. [15]

  1. https://www.uwezeshaji.go.tz/uploads/publications/sw1579593369-Mwongozo%20wa%20mafunzo%20VICOBA.pdf
  2. 1. https://www.simtrade.fr/blog_simtrade/vicoba/#:~:text=Village%20Community%20Bank%20(VICOBA),-Village%20Community%20Bank&text=The%20system%20started%20in%20Tanzania,set%20up%20joint%20economic%20projects.
  3. https://www.simtrade.fr/blog_simtrade/vicoba/#:~:text=Village%20Community%20Bank%20(VICOBA),-Village%20Community%20Bank&text=The%20system%20started%20in%20Tanzania,set%20up%20joint%20economic%20projects
  4. https://www.simtrade.fr/blog_simtrade/vicoba/#:~:text=Village%20Community%20Bank%20(VICOBA),-Village%20Community%20Bank&text=The%20system%20started%20in%20Tanzania,set%20up%20joint%20economic%20projects.
  5. http://kitegacc.org/campaigns/village-community-banking-vicoba/#:~:text=The%20VICOBA%20program%20has%20led,food%2C%20shelter%2C%20and%20education.&text=In%20terms%20of%20community%20development,are%20actively%20supporting%20local%20initiatives Ilihifadhiwa 22 Septemba 2023 kwenye Wayback Machine..
  6. http://kitegacc.org/campaigns/village-community-banking-vicoba/#:~:text=The%20VICOBA%20program%20has%20led,food%2C%20shelter%2C%20and%20education.&text=In%20terms%20of%20community%20development,are%20actively%20supporting%20local%20initiatives Ilihifadhiwa 22 Septemba 2023 kwenye Wayback Machine..
  7. https://www.researchgate.net/publication/365060316_THE_ROLE_OF_VILLAGE_COMMUNITY_BANKS_VICOBA_MICROCREDITS_IN_PROMOTING_SUSTAINABLE_MICRO_AND_SMALL_SCALE_INDUSTRIALIZATION_IN_KILIMANJARO_REGION_TANZANIA
  8. Joseph Magali. (2021), Wajibu wa Benki za Jumuiya ya Kijiji (Vicoba) Mikopo Midogo katika Kukuza Uendelezaji wa Viwanda Vidogo na Vidogo Endelevu katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania. Jarida la Elimu ya Biashara (BEJ), Juzuu ya I, Toleo la II, Kurasa 15. www.cbe.ac.tz/bej
  9. https://www.worldwildlife.org/stories/how-community-banking-empowers-women-in-tanzania
  10. https://www.wwf.or.tz/?35042/The-story-of-Fatuma-Mamcho-A-VICOBA-champion-Trailblazing-in-Mafia
  11. https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/makala/johari/vikoba-vimewainua-wanawake-wengi-nchini-2785432
  12. https://www.uwezeshaji.go.tz/uploads/publications/sw1579593369-Mwongozo%20wa%20mafunzo%20VICOBA.pdf
  13. https://www.uwezeshaji.go.tz/uploads/publications/sw1579593369-Mwongozo%20wa%20mafunzo%20VICOBA.pdf
  14. https://www.simtrade.fr/blog_simtrade/vicoba/#:~:text=Village%20Community%20Bank%20(VICOBA),-Village%20Community%20Bank&text=The%20system%20started%20in%20Tanzania,set%20up%20joint%20economic%20projects.
  15. https://kibaba.co.tz/docs/jinsi-mfumo-wa-vicoba-unavyofanya-kazi-tanzania/
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu VICOBA kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.