Uwanja wa michezo wa Pantami
Mandhari
Uwanja wa michezo wa Pantami una uwezo wa kuchua watu 12,000 [1].Uwanja huu unapatikana katika wilaya ya Pantami huko Gombe nchini Nigeria na unatumika kwa matumizi mbalimbali. Unatumika zaidi kwa mechi za mpira wa miguu lakini pia unatumika kuandaa hafla na sherehe mbalimbali kama vile sherehe za kiserikali,kidini,kisiasa na kijamii. Ni uwanja rasmi wa nyumbani wa timu ya mpira ya Gombe United F.C na umechukuliwa kama moja ya vituo vya kisasa vya michezo nchini humo. Ulifunguliwa mnamo mwaka 2010.
Muundo wa kiwanja hicho ni wa kujivunia kutokana na vifaa muhimu vitatu ambavyo vinachukua uwanja wa mpira wa miguu, wimbo wa riadha na uwanja wa mazoezi uliojengwa kwa ajili ya kukuza maendeleo ya michezo katika jimbo.[2]
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- http://naijaligue.blogspot.com/2010/08/gombe-utd-set-to-move-into-new-stadium.html http://naijaligue.blogspot.com/2010/08/gombe-utd-set-to-move-into-new-stadium.html
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ http://allafrica.com/stories/201105170902.html
- ↑ Abubakar, (Gombe), David Ngobua (Abuja) & Rabilu (2020-09-26). "N3bn Pantami stadium Gombe in dire need of maintenance". Daily Trust (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-12-18.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Pantami kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |