Uwanja wa michezo wa Moruleng

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uwanja wa michezo wa Moruleng pia unajulikana kama uwanja wa Saulspoort unatumika kwa matumizi mbalimbali na unapatikana kijiji cha Moruleng, sehemu ndogo ya wachimbaji wa madini takribani km 60 kutoka Mji wa Rustenburg nchini Afrika Kusini. Ulitumika zaidi kwa ajili ya mchezo wa mpira wa miguu na ni uwanja wa nyumbani wa timu ya mpira ya Platinum Stars. Uwanja huo ulikuwa sehemu ya mapendekezo ya jiji la Rustenburg kwa ajili ya Kombe la Dunia lililofanyika mwaka 2010 na pia ulitumika kama uwanja wa mazoezi wa timu zilizoshiriki katika kombe la Dunia katika shirikisho la FIFA mwaka 2009.

Uwanja huo ulijengwa na kampuni za Afrika Kusini Stefanutti Stocks na Omnistruct Nkosi kwa msaada wa wahandisi wa muundo wa Arup Group Limited wa Durban. Uwanja huo ulibuniwa na kampuni ya usanifu yenye makao yake mjini Durban Paton Taylor Architects, kufuata kanuni za FIFA, ulitumiwa kama uwanja wa mazoezi katika Kombe la Dunia. Wachunguzi wa mradi huu walikuwa BTKM - Bham Tayob Khan Matunda.

Uwanja huo ulijengwa na kabila la Bakgatla-Ba-Kgafela ambalo limetawanyika katika vijiji 32 kwenye mkoa wa Kaskazini Magharibi. Chanzo kikuu cha utajiri wa kabila ilo linatokana na madini ya platinamu.

Uwanja huo ulifunguliwa mnamo mwezi Septemba mwaka 2009 kwa mara ya kwanza na mechi kati ya Mochudi Center Chiefs ya Botswana na Platinum Stars F.C. ya Afrika Kusini.[1]

Mchezo wa kwanza Ligi Kuu ya Soka uliofanyika kwenye uwanja huo ilikuwa ni kati ya Platinum Stars, timu ambayo hutumia uwanja huo kama uwanja wa nyumbani, na Ajax Cape Town.[2]

uwanja huo ulitumiwa na timu ya kitaifa ya mpira wa miguu ya New Zealand kama uwanja wa mazoezi wakati wa Kombe la Shirikisho la FIFA la mwaka 2009.[2]

Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya England ilicheza na Platinum Stars kama mchezo wa kujiandaa kabla ya Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2010 mnamo Juni 7, na England ilishinda ushindi wa 3-0.[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Moruleng Stadium opens for business. Mmegi Online (29 September 2009). Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-03-07. Iliwekwa mnamo 7 June 2010.
  2. 2.0 2.1 Bakgatla-Ba-Kgafela. Bakgatla-Ba-Kgafela (29 October 2009). Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-03-06. Iliwekwa mnamo 7 June 2010.
  3. "World Cup 2010: Platinum Stars 0 England 3 match report", The Telegraph, 8 June 2010. Retrieved on 14 November 2020. 
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Moruleng kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.