Nenda kwa yaliyomo

Uwanja wa michezo Odi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uwanja wa michezo Odi ni uwanja wenye matumizi mengi huko Mabopane Afrika kusini , Gauteng, nchini Afrika Kusini. Unatumiwa zaidi kwa mechi za mpira wa miguu (soka). Uwanja huo una uwezo wa kuingiza takribani watu 60,000. Ulikuwa uwanja wa nyumbani wa timu ya Garankuwa United timu ya mpira wa miguu.

Uwanja wa ODI uko Mabopane kaskazini mwa ([Pretoria]), chini ya mamlaka ya Halmashauri ya Jiji la Tshwane.

Uwanja huo una eneo kubwa ambalo halijafunikwa.

Uwanja ulijengwa mwishoni mwa mwaka mwaka 1980 na unajivunia vifaa vingi, pamoja na uwanja wa mpira, mchezo wa [riadha] , hafla za uwanja kurusha mkuki, kutupa nyundo, nk),pia ina sehemu 2 za kubadilisha seti 4 za vyoo vya kiume / vya kike, vibanda 4, chumba cha kupumzika cha VIP na viti, chumba cha usalama, chumba cha waamuzi, chumba cha waandishi wa habari, chumba cha kudhibiti, ofisi za msimamizi, chumba cha jenereta, maduka, maeneo kadhaa ya michezo ya ndani, siti 4 ya juu na ofisi 4 za tiketi. Vituo vya eneo la nje ya uwanja ni pamoja na nyumba ya kilabu, nyumba ya watunzaji, korti za tenisi, mpira wa magongo, mpira wa wavu na viwanja viwili vya mazoezi ya mpira. Ubunifu wa uwanja huo karibu unafanana na ule wa Uwanja wa Mmabatho uliopo Mahikeng.[1]

  1. Davis, Kitty (2019-03-26). What Happened to South African Stadiums After 2010 FIFA World Cup Ilihifadhiwa 31 Oktoba 2023 kwenye Wayback Machine.. SA Stadiums. Retrieved 2020-04-09.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo Odi kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.