Nenda kwa yaliyomo

Uwanja wa kimataifa wa michezo wa Moi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi ni uwanja wenye shughuli mbalimbali huko Kasarani, maeneo ya nje ya Nairobi nchini Kenya. Uwanja huu una kiwango cha kukimu takribani watu 60,000. Uligharamiwa na Serikali ya China mnamo mwaka 1987 kwa ajili ya michezo yote ya Afrika iliyofanyika jijini Nairobi. Unatumika kwa sasa haswa kwa mechi za kandanda, Timu ya Taifa ya Kenya huchezea mechi zake nyingi za nyumbani hapa. Kando na uga wa kandanda, pia kuna uwanja unao kimu takribani watu 5,000 wa Gymnasium na ukumbi wa kuogelea kama sehemu ya Uwanja wa Kitaifa wa Mchezo wa Moi. Vilabu vya soka kama vile Mathare United na Tusker FC hutumia uwanja huu kwa mechi zao za nyumbani. Kuna uga wa mchezo wa kriketi na uwanja wa gofu zinazojengwa.

Sherehe za mwaka wa 2009 za MTV Africa Music Awards zilifanyikia hapa.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa kimataifa wa michezo wa Moi kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-10-22. Iliwekwa mnamo 2010-03-17.