Nenda kwa yaliyomo

Upembuzi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Upembuzi ni njia ya kuelekea ukweli katika falsafa kwa kuzingatia hoja mbalimbali zinazopingana ili kuona kila moja inasaidia vipi kufikia lengo.

Tofauti na mihadhara, ambapo mara nyingi wasemaji wanapambana kwa hisia kali ili kushinda, wanaofuata upembuzi wanashirikiana kuelewa mada kwa dhati.

Mbinu hiyo ilistawishwa na Sokrates katika shule ya Athene kwa jina la διαλεκτική, dialektikḗ, yaani "mbinu ya kujadili".

Mwanafunzi wake Plato aliieneza kwa vitabu vyake vilivyoitwa "Majadiliano".

Pengine upembuzi unafanywa na mtu mmoja tu akipima mwenyewe hoja zinazopingana.