Nenda kwa yaliyomo

Unsata

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

UNSATA (kifupi cha University Nursing Student Association of Tanzania) ni chama cha wanafunzi wa uuguzi Tanzania ambao wanasoma ngazi zote za uuguzi kuanzia cheti, stashahada, shahada na kuendelea ili mradi asiwe nje ya taratibu na maadili ambayo mwanafunzi wa uuguzi anapaswa kuwanayo. Chama kilianzishwa rasmi na kupata usajili chini ya wizara ya afya na kutambulika kwa mujibu wa sheria tarehe 8/05/2005.

Makao makuu yake yakiwa kwenye Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili

Malengo ya chama ni pamoja na:

  1. kuweza kuwaweka pamoja wanafunzi wauguzi kuzungumza na kuweza kutatua kero mbalimbali zinazowakabili
  2. kuweza kuhamasisha wanafunzi kuwa na mtazamo chanya juu ya uuguzi ilikuweza kutoa msaada katika jamii
  3. kuweza kuondoa fikra potofu juu ya wanaume wanaosoma hii kozi kwani imezoeleka kuwa ni kozi ya wanawake tu kwani ni mawazo potofu
  4. kuweza kuishi katka maadili ya uuguzi pamoja na upendo na amani
  5. kuweza kukitangaza chama kila kona ya Tanzania