Umoja wa Kimataifa wa Astronomia
Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (kifupi: UKIA) (kwa Kiingereza: International Astronomical Union - IAU au Union astronomique internationale, UAI) ni shirika la kimataifa linalounganisha mashirika ya wataalamu wa astronomia kutoka nchi mbalimbali. Lilianzishwa mwaka 1919 na ofisi yake iko mjini Paris, Ufaransa.
Shabaha ya umoja ni kuendeleza na kuhifadhi elimu ya astronomia. Wanachama ni wataalamu waliosoma sayansi hii na kufanya kazi ya uchunguzi na kufundisha katika vyuo vikuu au taasisi za astronomia. mwaka 2008 idadi ilikuwa wanachama 9623 katika nchi 86.
Umoja wa Kimataifa wa Astronomia unashirikiana na vikundi na shirika za wanaastronomia ridhaa zinazounganisha wapenzi wa astronomia wasiofanya kazi katika fani hii lakini kuangalia nyota kama ridhaa.
IAU ina wajibu wa kutawala mfumo wa kutoa majina ya magimba yanayoendelea kutambuliwa katika anga ya ulimwengu pamoja na majina ya milima au kasoko yao.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Website of the International Astronomical Union
- XXVIth General Assembly 2006 Archived 10 Aprili 2003 at the Wayback Machine.