Ugonjwa wa mgandamizo wa fumbatio
Ugonjwa wa mgandamizo wa fumbatio | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Faili:Abdominal ratio (Radiopaedia 66777) (cropped).jpeg | |
Kundi Maalumu | Utunzaji muhimu |
Dalili | Utoaji mkojo uliopunguka, tumbo gumu[1] |
Visababishi | Sepsis, kongosho, kutokwa na damu ndani ya tumbo, matumbo yaliyopanuka, kuungua, kiwewe cha tumbo, kiasi kikubwa cha maji ya mishipa[1] |
Sababu za hatari | Unene kupita kiasi, ujauzito, shinikizo la juu la kifua, kumweka mtu kwa mbele yake[1] |
Njia ya kuitambua hali hii | Shinikizo la juu la mrija wa Foley na kushindwa kwa viungo[1] |
Matibabu | Kudumisha shinikizo la juu la damu, mrija wa tumbo, neostigmine, laxatives, mrija wa mkundu, kutoa nje ascitis, upasuaji[1] |
Idadi ya utokeaji wake | Kiasi cha kawaida (ICU)[1] |
Vifo | 65%[2] |
Ugonjwa wa mgandamizo wa fumbatio (Abdominal compartment syndrome (ACS)) ni wakati tumbo linapata shinikizo la juu la ndani, na kusababisha kutofanya kazi kwa viungo.[1][3] Dalili zake zinaweza kujumuisha fumbatio lililovimba na gumu na kupunguka kutoka kwa mkojo.[1][2] Miongoni mwa wale ambao waliopitishiwa bomba la hewa kwenye trakea (intubated), uingizaji hewa unakuwa vigumu.[2] Matatizo yanaweza kujumuisha kushindwa kwa figo, kushindwa kupumua, kushindwa kwa moyo, utumbo wa kishemia (ulio na upungufu wa mzungu wa damu), na kuongezeka kwa shinikizo la ndani ya fuvu la kichwa; kuishia katika kushindwa kwa mfumo wa viungo vingi.[1][2]
Ugonjwa huu unaweza kutokea kama matokeo ya sepsis, kongosho, kutokwa na damu ndani ya fumbatio, matumbo yaliyopanuka au kuvimba, kuungua, majeraha ya tumbo au upasuaji, au kiasi kikubwa cha viowevu kupitia mishipa.[1][2] Mambo ambayo yanaweza kuzidisha hali hii ni pamoja na kunenepa kupita kiasi, ujauzito, shinikizo la juu la kifua, na kumweka mgonjwa kwa mbele yake.[1] Utaratibu wa msingi unahusisha shinikizo lililoongezeka, ambalo huathiri moyo, mapafu, figo na ubongo.[1] Utambuzi wake unaweza kuungwa mkono na kupima shinikizo la zaidi ya 20mm Hg kupitia katheta ya Foley iliyowekwa kwenye kibofu cha mkojo.[1]
Matibabu yake yanahusisha kuweka shinikizo la damu juu vya kutosha, huku ukipunguza viowevu vya kupitia mishipa, pamoja na juhudi za kupunguza shinikizo la tumbo.[1] Shinikizo la damu linalolengwa ni angalau 60 mm Hg juu ya shinikizo la ndani ya tumbo.[1] Shinikizo la tumbo linaweza kupunguzwa kwa mirija ya tumbo, neostigmine, laxatives au mrija wa mkundu, na kumwaga nje ascitis yoyote.[1] Ikiwa hili halitakuwa na ufanisi, upasuaji mzuri wa kufungua tumbo unaweza kufanywa.[1]
Ugonjwa wa sehemu ya tumbo hutokea kwa kawaida katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).[1] Hatari ya kifo ni kubwa kama 70%.[2] Ongezeko la shinikizo la tumbo lilielezewa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1863 na Etienne-Jules Marey, pamoja na uhusiano wake na kutofanya kazi kwa viungo vilivyobainishwa katika mwaka wa 1873.[4] Neno la sasa lilianza kutumika katika mwaka wa 1989.[4]
Marejeleo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 1.12 1.13 1.14 1.15 1.16 1.17 Farkas, Josh. "Abdominal compartment syndrome". IBCC. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Septemba 2022. Iliwekwa mnamo 7 Juni 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 Hacking, Craig. "Abdominal compartment syndrome | Radiology Reference Article | Radiopaedia.org". Radiopaedia. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Februari 2024. Iliwekwa mnamo 8 Juni 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Cheatham, Michael Lee (Aprili 2009). "Abdominal compartment syndrome". Current Opinion in Critical Care. 15 (2): 154–162. doi:10.1097/MCC.0b013e3283297934. ISSN 1070-5295. PMID 19276799. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-10-20. Iliwekwa mnamo 2022-02-05.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 4.0 4.1 Sanda, RB (Mei 2007). "Abdominal compartment syndrome". Annals of Saudi medicine. 27 (3): 183–90. doi:10.5144/0256-4947.2007.183. PMID 17568172.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)