Nenda kwa yaliyomo

Ufukwe wa Omaha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha maarufu iliyopewa jina la Ndani ya Taya za Mauti (Into the Jaws of Death) ikionyesha wanajeshi wa Marekani na washirika wake wakishuka kutoka katika chombo wakiwasilia katika fukwe ya Omaha.
Hapa wakiwa ndani ya maji tayari kwenda kukabiliana na majeshi ya Kijerumani.

Ufukwe wa Omaha likuwa mojawapo ya fukwe tano zilizotumika wakati wa Mapigano ya Normandy mnamo tarehe 6 Juni, 1944, wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, tukio maarufu kama D-Day.

Uvamizi huu ulifanywa na vikosi vya washirika wakiongozwa na Marekani, Uingereza, Kanada na mataifa mengine ya Muungano ili kuanzisha mashambulizi makubwa dhidi ya Ujerumani ya Kinazi ambayo ilikuwa imevamia maeneo mengi ya Ulaya. Ufukwe wa Omaha lilikuwa eneo la kusini mwa Jangwa la Normandy huko nchini Ufaransa. Wakakti huo lilikuwa chini ya ulinzi mkali wa Wajerumani waliokuwa wameweka kambi yenye ulinzi mkali. Eneo lilizungushiwa kwa maboma, mizinga, mitego, minara ya ulinzi na mabomu yaliyozikwa ardhini.

Uvamizi huu ulifanywa na wanajeshi wa Marekani kutoka Divisheni ya 1 na Divisheni ya 29, wakisaidiwa na meli za kivita na ndege za washirika.

Pamoja na uvamizi huu, kuwasili kwa wanajeshi kwenye fukwe kulikumbwa na matatizo mengi. Ikiwa ni pamoja na hali mbaya ya hewa, mawimbi makali, na vizuizi vingi vya kiulinzi vilivyowekwa na Wajerumani. Wakati wakiwasili kwenye fukwe, wanajeshi walikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa vikosi vya Ujerumani vilivyojificha kwenye ngome na milima inayozunguka fukwe hizo. Mapigano hayo yalikuwa ya kinyama sana. Wanajeshi wengi walipoteza maisha kutokana na mashambulizi makali ya risasi kutoka kwa wanajeshi wa Kijerumani. Achilia mbali mitego na milipuko ya mabomu iliyofutikwa ardhini.

Hadi wanafanikiwa kulitwa eneo la fukwe, takribani wanajeshi wa Marekani walipoteza maisha zaidi ya watu 2,000 katika mapigano ya siku moja pekee. Uvamizi wa Omaha ulikuwa mojawapo ya hatua muhimu zaidi za mabadiliko katika Vita ya Pili ya Dunia na ulifanya kuwa mwanzo wa mwisho wa utawala wa Ujerumani ya Nazi barani Ulaya.

Hadi leo, Omaha inabaki kuwa kumbukumbu ya mashujaa na kujitoa kwa kiasi kikubwa kwa wanajeshi washirika kwa ajili ya uhuru wa dunia. Eneo hili ni sehemu ya kumbukumbu ya vita, ambapo makaburi na makumbusho yamejengwa ili kuenzi wanajeshi waliokufa, pamoja na kuwapa heshima wale waliopigana na kushinda vita dhidi ya utawala wa kiimla wa Nazi.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Kigezo:Battle of Normandy