Udongo ulioshindiliwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Udongo unashindiliwa, ujenzi nchini Vietnam
Nyumba ya udongo ya mwaka 1836 iko mjini Weilburg, Ujerumani
Ubunifu wa udongo ni mvutio wa kitalii pale Sana'a, Yemen

Udongo ulioshindiliwa (ing. rammed earth) ni mbinu ya ujenzi iliyowahi kubuniwa katika enzi za kale na kuangaliwa upya leo hii kwa sababu ya faida zake.

Hii ni mbinu tofauti na kutumia matofali yasiyochomwa, pia tofauti na ukuta wa udongo bila kushindilia.

Namna ya kutumia udongo ulioshindiliwa[hariri | hariri chanzo]

Udongo humwagwa ndani ya kalibu ya ubao kisha hushindiliwa kwa kuipiga kwa miguu au kwa mpini. Kwa kwa kutumia njia hii, kuta za nyumba zinaweza kujengwa mfululizo kwa kuhamisha kalibu tu, au bloku zinatengenezwa zinazotumiwa kama matofali makubwa.

Kwa kawaida udongo unashindiliwa katika matabaka yenye unene wa sentimita 10-40. Udongo unaofaa ni wa kunata kiasi (usiwe mchanga—mchanga, si lazima kuwa na ubora wa ufinyanzi). Usiwe m'bichi mno. Kalibu inatengenezwa kwa kutumia ubao. Lazima kuwawapo na uthabiti ili kuhimili vishindo wakati wa kushindilia. Siku hizi wanatumia pia mashine ya kushindilia.

Unene wa ukuta ndani ya jengo uwe angalau sehemu ya 12 ya urefu wake; yaani ukuta mwenye urefu wa mita 2.5 uwe na unene wa sentimita 21 au zaidi. Ukuta unaosimama nje ya jengo uwe mnene zaidi.

Faida na hasara[hariri | hariri chanzo]

Faida za mbinu hii ni gharama ndogo na matumizi kidogo ya nishati. Matokeo yake ni majengo imara yanayoweza kudumu miaka tele, katika mazingira makavu sana hata miaka maelfu. Faida nyingine ni tabianchi ndani ya vyumba vyake.

Hasara ni hatari ya kuingia kwa maji ndani ya ukuta. Jengo la aina hii linahitaji uangalifu kiasi kuhusu ubora wa paa lake. Vilevile majengo haya si imara sana katika mazingira yenye tetemeko la ardhi. Maafa makubwa yalitokea Agadir (Moroko) mwaka 1960 na Bam (Iran) mwaka 2003 ambako tetemeko la ardhi liliharibu mji wenye majengo mengi ya udongo ulioshindiliwa.

Ujenzi wa kisasa unaotumia udongo ulioshindiliwa unaimarisha majengo kwa vyuma.

Mifano[hariri | hariri chanzo]

Mifano ya kihistoria ya ubunifu unaotumia udongo ulioshindiliwa ni miji ya kihistoria kama Sanaa (Yemen) au Ait Benhaddou (Moroko).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]


Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.