Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1872
Mandhari
Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1872 ulikuwa wa 22 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 5 Novemba. Upande wa "Republican Party", Rais Ulysses Grant (pamoja na kaimu wake Henry Wilson) alimshinda mgombea wa "Democratic Party" Horace Greeley (pamoja na kaimu wake Benjamin Brown).
Matokeo
[hariri | hariri chanzo]Grant akapata kura 286, na Greeley 66 katika uchaguzi wenyewe. Lakini Greeley alifariki tarehe 29 Novemba kabla ya wachaguzi kupiga kura. Kwa hiyo, wanachama wa "Democrats" wanne wengine wakapata kura mbalimbali, baadhi yao Brown, Thomas Hendricks, David Davis na Charles Jenkins. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |