Nenda kwa yaliyomo

Ubuntu Hub

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ubuntu Hub ni asasi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa mkoani Arusha [1] kwa lengo la kuwasaidia wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo wanaopatikana katika mkoa huo.

Asasi hiyo ilianzishwa na Collins Kimaro pamoja na wenzake wawili ambao ni Carolin Kandusi [2] na Jonathan Ruta.

Ubuntu wamekuwa wakiandaa mafunzo mbalimbali na elimu kwa ajili ya kuwaelimisha wafanyabiashara na wajasiriamali wanaochipukia katika mbinu bora za kukuza na kupata mawazo ya biashara pamoja na kuwaendeleza katika sekta ya ubunifu.

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-11-29. Iliwekwa mnamo 2021-01-22.
  2. https://tanzania.dotrust.org/story/carolyn/