Uandishi wa ripoti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Ripoti ni maelezo yanayotolewa kama taarifa juu ya mtu, kitu au tukio fulani ambalo limetokea, kwa mfano ajali, kifo na kadhalika.

Ripoti huandikwa kwa madhumuni ya kutoa taarifa ili taarifa hiyo iweze kufanyiwa kazi au walau kuhifadhiwa kama kumbukumbu.

Aina za ripoti[hariri | hariri chanzo]

Muundo wa ripoti[hariri | hariri chanzo]

Ripoti sharti lake ni kwamba iwe na sehemu kuu nne; sehemu hizo ni:

1. Kichwa cha ripoti Ripoti lazima iwe na kichwa cha habari; kichwa hicho huandikwa kwa maelezo machache. Mambo muhimu yanayotakiwa kuwepo katika kichwa cha ripoti ni:

  • mahali pa tukio
  • aina ya tukio
  • tarehe ya tukio
  • muda wa tukio

2. Utangulizi wa ripoti Utangulizi wa ripoti hueleza kwa muhtasari lengo la ripoti kama ni kutoa taarifa au kumbukumbu. Majina ya wanajopo pia hutajwa kulingana na idadi uliyopewa kwenye swali.

3. Kiini cha ripoti Kiini cha ripoti kina maelezo yote kuhusiana na tukio lenyewe; sehemu hii huelezea kwa ufasaha mambo yaliyotokea, chanzo chake, ukubwa wake, wahusika, na tukio linalohusika.

4. Mwisho wa ripoti Hii ni sehemu ya mwisho ya ripoti. Sehemu hii huonyesha mambo makuu mawili:

Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uandishi wa ripoti kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.