Nenda kwa yaliyomo

UNAMIR

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Nchini Rwanda (UNAMIR), ilianzishwa tarehe 5 Oktoba 1993[1] ili kutekeleza Makubaliano ya Arusha, ambayo ilikubaliwa ili kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Rwanda. Ujembe ilitendeka mwezi Oktoba mwaka 1993 hadi mwezi Machi mwaka 1996. Licha ya nia yake nzuri, UNAMIR haikuweza kufikia malengo yake. Kutofaulu hii kulisababishwa na uongozi mbaya, mamlaka yasiyo dhahiri, na rasilimali zisizotosheleza. Kwa sababu hii, miezi michache baada ya ujembe, mauaji ya kimbari ya Rwanda ilianza tarehe saba mwezi wa nne mwaka wa 1994.

Matukio ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Oktoba mwaka 1993, vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Rwanda vilianzishwa na chama cha Uzalendo cha Rwanda (Rwanda Patriotic Front-RPF) kutoka Uganda kusini. Wakiongozwa na Fred Rwigyema na Paul Kagame, kundi la RPF lilikuwa na wanajeshi zaidi ya elfu nne. Kwa sababu ya kuungwa mkono na serikali ya Uganda, shambulizi la kwanza la RPF lilizuiliwa kwa sababu serikali za Ufaransa na Kongo ziliunga mkono serikali ya Hutu na rais wao Juvenal Habyarimana. Baada ya uvamizi kuzuiliwa, RPF walirudi nyuma hadi milima ya Virunga katika kaskazini magharibi mwa Rwanda. Katika miaka iliyofuata, wapiganaji ya RPF walipigana vita vya msituni kutoka yalipokuwa maficho yao katika milima ya Virunga. Mwishowe, mazungumzo ya amani katika mji wa Arusha nchini Tanzania, lilizaa Makubaliano ya Arusha ambayo iliyopendekeza utawala wa pamoja na msaada kutoka Umoja wa Mataifa. Ombi hii liliongoza kwa UNAMIR.

Uanzishwaji

[hariri | hariri chanzo]

UNAMIR ilianzishwa na kupewa majukumu ifuatayo:

  • Kulinda mji wa Kigali
  • Kuangalia makubaliano ya kusimamisha mapigano
  • Kusaidia na katika uondoaji wa mabomu ya kutega
  • Kupeleleza ukiukwaji wa Makubaliano ya Arusha
  • Kusaidia fatica masuala ya wakimbizi
  • Kuangalia vitendo vya Polisi wa Rwanda

[2]

Muundo wa jeshi la kulinda amani

[hariri | hariri chanzo]

Kamanda wa kwanza wa misheni alikuwa Generali Romeo Dallaire kutoka Kanada. Kamanda wa pili alikuwa Meja Generali Guy Tousignant, pia kutoka Kanada. Waliomba wanajeshi elfu nne na mia tano, lakini walipokea askari elfu mbili na mia tano tu. Ubeljiji, Bangladesh, Ghana, na Tunisia walisaidia kutuma wanajeshi pia.

Utendakazi kabla ya mauaji ya kimbari

[hariri | hariri chanzo]

UNAMIR ilipangwa miezi saba kabla ya mauaji ya kimbari. Wakati huo, Kamanda Dallaire alielewa kwamba serikali ya Hutu haikuwa inafuata Makubaliano ya Arusha.[3] Kamanda Daiilre alitoa habari kuhusu mauaji ya kimbari ambayo yalikuwa yanakaribia, lakini uongozi wa Umoja wa Mataifa haukutaka kuchukua hatua. Uamuzi huu uliweka UNAMIR katika hali ngumu.

Mauaji ya kimbari

[hariri | hariri chanzo]

Tarehe sita mwezi wa nne mwaka wa 1994, ndege ya rais Habyarimana ilitunguliwa ikikaribia Kigali. Mauaji ya Kimbari ilianza mara moja kwa kishindo. Nchi iliporomoka usiku kucha na watu wa Watusi walianza kuchinjwa. Wanajeshi kumi wa kueka amani wa UNAMIR waliuawa katika siku ya kwanza. UNAMIR walilazimika kutazama tu. Baada ya vifo vya  wanajeshi wa Ubelgiji, baadhi ya nchi ziliamuru wanajeshi wao kurudi nyumbani. UNAMIR ilivunjika kabisa. Wao walifanya walichoweza, lakini hawangeweza kusaidia Watutsi wote. Katika siku mia moja, karibu watu milioni moja waliuawa.[4] Mwezi wa sita mwaka wa 1994, Umoja wa Mataifa hatimaye ulikubali kuimarisha UNAMIR, lakini ulikuwa umechelewa kwa sababu chama cha RPF kilikuwa na mamlaka.

Katika historia

[hariri | hariri chanzo]

UNAMIR ilijulikana kwa kushindwa kabisa kutekeleza majukumu yake. Rwanda ilikuwa nchi kubwa ambayo ilitangulia kuwa na mauaji ya kimbari na uongozi ya Umoja wa Mataifa ulijuta kukosa kutenda kwa usahihi. Kushindwa kwa UNAMIR kulibadili uwekaji amani wa Umoja wa Mataifa daima. Umoja wa Mataifa sasa uko makini zaidi.

  1. "UNAMIR". peacekeeping.un.org. Iliwekwa mnamo 2022-04-19.
  2. "UNAMIR". peacekeeping.un.org. Iliwekwa mnamo 2022-04-19.
  3. "Roméo Dallaire | Canadian military officer | Britannica". www.britannica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-19.
  4. World History Edu (2020-12-20). "Rwandan Genocide – Summary, Death Toll, & Facts". World History Edu (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-04-19.