Tuzo ya Sao Paulo ya Fasihi
Mandhari
Tuzo ya Sao Paulo ya Fasihi (kwa Kireno: Prêmio São Paulo de Literatura) ni tuzo ya fasihi ya Brazil ambayo hutolewa kwa ajili ya riwaya zilizotungwa kwa lugha ya Kireno na kuchapishwa nchini Brazil. Tuzo hii ilianzishwa mnamo mwaka wa 2008 na Waziri wa Utamaduni wa Jimbo la São Paulo. Ijapokuwa si la kale sana kama jinsi zilivyo tuzo zingine za fasihi huko nchini Brazili kama Prêmio Machado de Assis.
Tuzo hii ya São Paulo imechupukia haraka zaidi na kupata sifa kubwa mno. Kwa mfano, mwaka wa 2011, kulikuwa na mawasilisho 221 kwa ajili ya ugawaji wa tuzo.[1]
Washindi
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Kitabu Bora ya Mwaka | Kitabu Bora ya Mwaka - Mwandishi Chipukizi | ||
---|---|---|---|---|
Kichwa | Mtunzi | Kichwa | Mtunzi | |
2008 | O Filho Eterno | Cristóvão Tezza | A Chave de Casa | Tatiana Salem Levy |
2009 | Galiléia | Ronaldo Correia de Brito | A Parede no Escuro | Altair Martins |
2010 | A minha alma é irmã de Deus | Raimundo Carrero | Se eu fechar os olhos agora | Edney Silvestre |
2011 | Passageiro do Fim do Dia | Rubens Figueiredo | Método Prático da Guerrilha | Marcelo Ferroni |
2012 | Vermelho Amargo | Bartolomeu Campos de Queirós | Os Hungareses | Suzana Montoro |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "R$200,000 São Paulo Literary Award Shortlist Announced". Publish News Brazil. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-07-21. Iliwekwa mnamo 16 Machi 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)