Tuul (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Tuul (Kimongolia: Туул гол) ni mto muhimu wa Mongolia. Mto una urefu wa km 704 na beseni ya km² 49,840.

Chanzo chake ni ambapo tawimito ya Namiya na Nergui inaungana kwenye mtelemko wa mlima Khentei. Tuul inapeleka maji yake kwenda ziwa Baikal kupitia mto Selenge. Inapita katika mji mkuu Ulanbaatar.

Beseni ya Tuul ni asilimia 3.19 za eneo la Mongolia tu lakini zaidi ya nusu ya wakazi wa nchi huishi humo.


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Kuhusu beseni ya Tuul