Trine Haltvik

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Trine Haltvik (amezaliwa Machi 23, 1965) ni kocha wa mpira wa mikono kutoka Norwei na mchezaji wa zamani wa mpira wa mikono. Kwa sasa ni kocha wa timu ya wasichana ya Norwei chini ya umri wa miaka 17.

Haltvik alianza uchezaji wa mpira wa mikono akiwa na miaka 16 pekee katika klabu ya Byåsen IL, alitarajiwa kucheza mwaka mmoja kwenye timu ya Remudas Gran Canaria nchini Uhispania, alibaki katika klabu hiyo. Uaminifu wake na ukongwe wake kwenye taaluma yake, umempa jina la utani "Mor" au "Mother" ikimaanisha Mama. Ameichezea timu ya taifa ya Norwei katika michezo 241, akifunga mabao 834.[1]

Alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Dunia wa 1998 na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Mikono.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "404 | handball.no". handball.no - Norges Håndballforbund (kwa Norwegian). Iliwekwa mnamo 2023-07-30. 
  2. "International Handball Federation". web.archive.org. 2007-05-20. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-05-20. Iliwekwa mnamo 2023-07-30.