Nenda kwa yaliyomo

Trifaroteni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Trifaroteni (Trifarotene), inayouzwa chini ya jina la chapa Aklief, ni dawa inayotumika kutibu chunusi.[1] Dawa hii inatumika kwa ngozi kama krimu.[1] Mafuta ya kulainisha ngoozi (Moisturizer) pia yanaweza kutumika kuzuia kuwasha kwa ngozi.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuwashwa, kusumbuliwa na kuchomwa na jua kwa urahisi.[1] Kuna wasiwasi kwamba matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto.[2] Ni retinoidi(retinoid), yaani kemikali zenye vitamini A zinayotunza ngozi; hasa retinoidi teule za kizazi cha nne za kipokezi cha agonisti ya asidi ya retinoic (RAR) -γ.[1][3]

Trifaroteni iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani, Kanada, na Ulaya mwaka wa 2019.[1][2] Nchini Marekani, mrija wa gramu 45 hugharimu takriban dola za Kimarekani 575 kufikia mwaka wa 2021.[4]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Trifarotene Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 19 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 "Australian Public Assessment Report for Trifarotene" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 23 Septemba 2021. Iliwekwa mnamo 19 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Scott LJ (Novemba 2019). "Trifarotene: First Approval". Drugs. 79 (17): 1905–1909. doi:10.1007/s40265-019-01218-6. PMID 31713811. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 26 Juni 2021.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Aklief Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Machi 2024. Iliwekwa mnamo 19 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Trifaroteni kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.