Traveler

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Traveler
Aina Maigizo, Kutisha
Imetungwa na David DiGilio
Nyota Aaron Stanford
Matthew Bomer
Logan Marshall-Green
Nchi inayotoka Marekani
Lugha Kiingereza
Ina misimu 1
Utayarishaji
Watayarishaji
wakuu
Bruce Cohen
Dan Jinks
Charles Grant Craig
Mtayarishaji
msaidizi
Vanessa Reisen
Muda makisio ni dk. 42
Urushaji wa matangazo
Kituo ABC
Inarushwa na 10 Mei 2007
Viungo vya nje

Traveler ni tamthiliya ya Marekani iliyodumu kwa muda mfupi ikianza kurushwa hewani 10 Mei 2007 hadi 18 Julai 2007 kupitia ABC, Marekani. Traveler ilitayarishwa na Warner Bros. Television.

Traveler ilisimamishwa rasmi baada ya episodi nane za kwanza, 18 Julai 2007. Mashabiki walijaribu kuinusuru tamthilia bila mafanikio. David DiGilio, mtunzi, ili kujibu maswali, 28 Septemba 2007, aliandaa "blogu"[1] ambayo ilithibitisha kusimimamishwa rasmi kwa Traveler.

Muhtasari[hariri | hariri chanzo]

Tamthiliya inaanzia kwa Jay Burchell na Tylor Fog, wahitimu wa Yale University waliojikuta wakituhumiwa kuhusika na ulipuaji wa makumbusho ya Drexler, New York. Inaonekana rafiki yao, Will Traveler (p.a.k Daniel Taft) amewachezea shere waonekane ni magaidi waliohusika na ulipuaji. Baada ya mlipuko, Traveler anatoweka na hakuna ushahidi wowote unaodhihirisha uwepo wake duniani.

Jay na Tyler wanawakimbia FBI, sababu inayopelekea waonekane kuwa magaidi wazalendo. Wanamkimbilia baba wa Tyler, Carlton, lakini anawashauri watokomee. Wakiwa nje ya mji wao, Jay na Tyler wanachunguza maisha ya nyuma ya Will Traveler wakitumai kuambulia chochote kusafisha majina yao.

Muda huohuo, Traveler, akiwa hai na mwenye afya tele, naye pia anatafuta ukweli. inakuja kujulikana kuwa Traveler ni askari akikitumikia kitengo cha Usalama wa Taifa la Marekani kiitwacho Fourth Branch, na taratibu siri nzito inafichuka.

Jay na Tyler wanaungana na Will katika sehemu ya saba, msimu wa kwanza wa tamthiliya, na kwa pamoja wanajaribu kuwafikisha katika mkondo wa sheria wale wanaohusika na matatizo yao. Wanafanikiwa kumteka nyara Jack Freed, muongozaji wa Fourth Branch, lakini kabla ya kumtumia kusafisha majina yao, gari alimokuwemo Freed linalipuka.

Wahusika[hariri | hariri chanzo]

Kwa ujumla Traveler inaangaza hasa juhudi za Jay Burchell (Matthew Bomer) na Tyler Fog (Logan Marshall-Green), wahitimu wenye jukumu la kuhakikisha wanasafisha majina yao katika jamii baada ya kupakaziwa tuhuma za kulipua makumbusho na rafiki yao Will Traveler (Aaron Stanford).

Jay na Tyler wanagundua kuhusika kwa Jack Freed (Neal McDonough) kutoka usalama wa taifa na pia Carlton Fog (William Sadler), baba wa Tyler na mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa. The Porter (Billy Mayo) anwaisaidia Tyler na Jay. Kim Doherty (Pascale Hutton), mchumba wa Jay, inamlazimu akubaliane na maisha ya kusumbuliwa na FBI pamoja na hadhara.

Baadaye katika sehemu ya New Haven, inadhihirika kuwa Will Traveler yu hai. Sonja Bennett amecheza kama Maya (mchumba wa Will).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. DiGilio, David (2007-09-28). "Closure". David's Traveler Blog. TV Guide. Iliwekwa mnamo 2008-08-26. {{cite web}}: Check date values in: |date= (help); Italic or bold markup not allowed in: |publisher= (help)

Viungo vyanje[hariri | hariri chanzo]