Tracy Ainsworth

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tracy Ainsworth ni mwanabaiolojia wa masuala ya baharini na Profesa wa Sayansi katika Chuo Kikuu cha New South Wales, anayefanya kazi za utafiti wa miamba ya matumbawe. Utafiti wake pia unahusu baiolojia ya seli, magonjwa, na kinga. Alitunukiwa nishani ya Dorothy Hill ya sayansi kutoka Chuo cha Sayansi cha Australia( Australian Academy of Science), kutokana na utafiti wake juu ya miamba ya matumbawe, mikazo pamoja na athari za halijoto kwenye afya ya matumbawe.[1]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Taaluma ya Ainsworth imechunguza athari za kimazingira kwenye matumbawe, hasa matumbawe yanayojenga miamba, pamoja na mwingiliano baina ya viumbe.[2] Pia anasoma mfumo wa viumbe wanaotegemea viumbe wengine(symbioses) na milipuko ya magonjwa. Utafiti wake kuhusu bakteria wanaopatikana kwenye miamba ya matumbawe ulitoa ujuzi kuhusu mifumo ya magonjwa ya matumbawe, jinsi yanavyotokea na nini huyafanya yaendelee..[3]

Ainsworth pia amebainisha aina mbalimbali za bakteria wanaopatikana ndani ya seli ambazo zinaweza kuwa na mchango kwenye matumbawe. Pia amechunguza athari za kuongezeka kwa joto, na mabadiliko ya hali ya hewa, na namna itakavyo athiri matumbawe kwa sasa, na baadaye. Ainsworth amechapisha tafiti kuhusu athari za kupanda kwa joto la maji kwenye matumbawe..[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Aus Coral Reef Soc". 10 September 2018.  Check date values in: |date= (help)
  2. "Reef Matters Seminar Series: Prof. Tracy Ainsworth and Dr /ref> Coulson Lantz". Australian Coral Reef Society (kwa en-AU). 2021-05-07. Iliwekwa mnamo 2022-04-14. 
  3. "Tracy Ainsworth". Reef Restoration and Adaptation Program (kwa en-AU). Iliwekwa mnamo 2022-04-14. 
  4. Leggat, William; Heron, Scott; Fordyce, Alexander; Suggett, David; Ainsworth, Tracy (2022-01-01). "Experiment Degree Heating Week (eDHW) as a novel metric to reconcile and validate past and future global coral bleaching studies". Journal of Environmental Management 301: 113919. PMID 34731944 Check |pmid= value (help). doi:10.1016/j.jenvman.2021.113919.  Unknown parameter |s2cid= ignored (help)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tracy Ainsworth kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.