Tishiko King

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tishiko King anatoka Kisiwa cha Yorke kwenye visiwa vya Torres Strait vya Australia . Yeye ni mkurugenzi wa kampeni ya Seed Indigenous Youth Climate Network na alishiriki 2021 United Nations Climate Change Conference (COP26) huko Glasgow, ambapo pia aliwakilisha shirika la kisiwa cha Torres Strait, Our Islands Our Home. [1] [2]

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

King, Mwenyeji wa Australia, ni mwanamke wa Kulkalaig kutoka Kisiwa cha Masig (Kisiwa cha Yorke) na ana muunganiko wa kifamilia kati ya Kisiwa cha Badu na Mlango -Bahari wa Torres. Aliondoka nyumbani kwao na kwenda kusoma shule ya bweni akiwa na umri mdogo na alikulia kwenye mji wa watu wanaojuhusisha na migodi. Aliona athari za uchimbaji madini kwa wamiliki wa jadi. Baada ya mwaka mmoja wa masomo ya shahada ya kwanza, aliacha chuo kikuu na kufanya kazi kwenye kituo cha Kisiwa cha Moreton, kaskazini mashariki mwa Brisbane, ambapo aliimarisha upendo wake wa bahari. Uamuzi wake wa kutafuta kazi kama mwanabiolojia wa baharini ulichangiwa zaidi na Kimbunga Hamish mnamo 2009 ambacho kilisababisha uharibifu wa meli ya MV Pacific Adventurer, na kusababisha kumwagika kwa mafuta na makontena ya nitrati ya ammoniamu kwenye Bahari ya Coral, ambayo ilisombwa na pwani kwenye Kisiwa cha Moreton na maeneo ya jirani. King alikuwa sehemu ya wafanyakazi wa kusafisha kwenye Kisiwa cha Moreton, na kulimwezesha kujionea uharibifu uliosababishwa kwenye ukanda wa pwani na kwa viumbe vya baharini. [3] [4]

Marejeleo[hariri | hariri chanzo]

  1. ‘Indigenous people feel the climate crisis. Our land is a part of us’. The Age. Iliwekwa mnamo 15 November 2021.
  2. Our Islands Our Home. Our Islands Our Home. Iliwekwa mnamo 15 November 2021.
  3. Tishiko King, Seed Mob. Groundswell. Iliwekwa mnamo 15 November 2021.
  4. TISHIKO KING. World Science Festival. Iliwekwa mnamo 15 November 2021.

Kiungo cha nje[hariri | hariri chanzo]