Timazi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Timazi huonyesha kama ukuta ni wima au la
Mjenzi anapima wima kwa timazi kabla ya kumwaga simiti

Timazi ni kifaa cha ujenzi kinachosaidia kujenga ukuta kiwima-wima.

Kimsingi ni kitu kidogo na kizito kama jiwe, kipande cha metali ya risasi au chuma kilichofungwa kwa kamba. Uzito wa uzani utanyosha kamba kuwa nyoofu. Timazi ikitundikwa kando la ukuta inaelekea chini kiwima. Hapo kamba inatakiwa kwenda sambamba kabisa na ukuta. Baada ya kuweka timazi mjenzi anaona kama kuna tofauti au la. Picha naonyesha mfano wa ukuta wima (upande wa kushoto) na usio wima (upande wa kulia).

Katika ujenzi wa kisasa kuna mitambo inayochukua nafasi ya wima ya kawaida.

Matumizi mengine[hariri | hariri chanzo]

Usafiri kwa maji[hariri | hariri chanzo]

Kifaa ambacho ni sawa na timazi inatumiwa pia na mabaharia kwa kupima kina cha maji. Ila tu hapa hawaangalii kama kitu ni wima; wanapima kina cha maji kwa kutupa uzani uliofunga kwa kamba katika maji na kuona ni mita au futi ngapi za kamba zinazoingia hadi uzani unafika mwisho. Hii inasaidia wakati meli inakaribia pwani au kisiwa kuona kama kina kinatosha.

Fizikia[hariri | hariri chanzo]

Katika fizikia tabia ya timazi ya kumbembea (ing. pendulum) ilitumiwa kufanya utafiti wa graviti. Galileo Galilei alikuwa mtaalamu wa kwanza aliyechungulia tabia za timazi wakati wa kubembea na hisabati katika mwendo huu. Timazi ya kubembea (pendulum)