Nenda kwa yaliyomo

Daily Nation

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka The Daily Nation)

Daily Nation ni gazeti la kila siku nchini Kenya inayotolewa mjini Nairobi kwa lugha ya Kiingereza. Inauza takriban nakala 205,000 kila siku hivyo ni gazeti lenye wasomaji wengi katika Afrika ya Mashariki.

Gazeti hili ni sehemu ya kampuni ya hisa ya Nation Media Trust na hisa nyingi zinashikwa na Shirika la Aga Khan.

Taifa na Nation

[hariri | hariri chanzo]

Chanzo cha Daily Nation kilikuwa gazeti la Kiswahili "Taifa" lililoanzishwa mwaka 1958 na Mwingereza Charles Hayes kama gazeti la kila wiki. Kampuni yake ilinunuliwa na Karim Aga Khan IV mwaka 1959 kwa nia ya kuifanya gazeti la kila siku lililoitwa "Taifa leo".

1960 Taifa leo ilianza kupatikana kila siku. Tar. 3 Oktoba 1960 Daily Nation ilifuata kama toleo lake la Kiingereza.

Magazeti dada

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje na marejeo

[hariri | hariri chanzo]