Nenda kwa yaliyomo

The Crimson Wing: Mystery of the Flamingo(filamu)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

The Crimson Wing: Mystery of the Flamingos ni filamu iliyo toka mwaka 2008, ambayo inachunguza mkusanyiko mkubwa wa flamingo wadogo ambao hutokea kila mwaka katika Ziwa Natron nchini Tanzania na kando ya maziwa ya chumvi ya Bonde la Ufa la Afrika. Ilikuwa ni filamu ya kwanza iliyotolewa chini ya lebo ya filamu ya wakati huo ya kampuni ya Disneynature kupitia Walt Disney Studios Motion Pictures. Ilionyeshwa kwa mara ya kwanza nchini Ufaransa tarehe 26 Oktoba 2008, na simulizi la Zabou Breitman. Filamu hiyo ilitolewa katika kumbi za sinema nchini Uingereza tarehe 29 Septemba 2009 na moja kwa moja hadi video nchini Marekani tarehe 19 Oktoba 2010 na simulizi la Mariella Frostrup.

Muhutasari

[hariri | hariri chanzo]

Filamu hii ina husu maisha ya flamingo wadogo kandokando ya ziwa Natron nchini Tanzania, ikionyesha tabia ya kuzaliana na malezi ya aina hiyo ya ndege. Baada ya kujamiiana kwenye kisiwa kikubwa chenye chumvi nyingi, flamingo huzalisha vifaranga wao, ambao hujifunza kuishi na kukua katika mazingira hatarishi. Katika safari zao, wanakutana na korongo wa marabou ambao huwinda mayai na vifaranga wapya wanaozaliwa na fisi mwenye madoadoa ambao hawahurumii flamingo waliokomaa [1] .

  1. Crimson Wing: Mystery of the Flamingos [Original Motion Pic (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2024-05-04
Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu The Crimson Wing: Mystery of the Flamingo(filamu) kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.