Tessy Chocolate

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

"Kayitesy Abdul Kayondo" (7 Mei, 1996) ni jina la kutaja mjasiriamali wa vipodozi na mwanamitandao maarufu anayetambulika zaidi kwa jina la Tessy Chocolate kutoka nchini Tanzania. Umaarufu wake ulikuja katika nadhari ya umma ni baada ya kuzaa na mwimbaji mashuhuri wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Flava), Aslay[1]—ambaye amezaa naye mtoto mmoja aliyetambulika kwa jina la Mozzah Aslay. Hata hivyo, kwa sasa hawapo pamoja.

Tessy ameendelea kubaki na taji lake la umaarufu na hata kufungua kampuni ya viambata vya urembo. Biashara iliyopata uhai mnamo 23 Machi, 2019. Zaidi ilijikita katika kupara wajihi wa watoto wa kike. Ilichukua wingu la mwaka mmoja kufanya mapinduzi makubwa ya kiofisi yaliyopelekea kupata sifa kadha wa kadha.

Isivyo bahati, miezi miwili mbele, yaani, 13 Me, 2020, ofisi ilivunjwa na watu wasiojulikana na kuharibiwa vibaya mno. Kwa vile alikusudia kufukuzana kwa nguvu zote na kivuli cha urembo, hatimaye akaanzisha kipodozi kingine kilichoitwa jina la Momo Beauty[2].[3] Hili lilileta shani ya kufunguliwa duka lingine la vipodozi vya ngozi.

Mara kadhaa amekuwa akikiri kuwa Aslay amekuwa na mchango mkubwa kufikia hapa alipo leo. Tessy ni mahuluti wa Kichaga (mama) na Kitusi (baba).[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]