Nenda kwa yaliyomo

Tessa Thompson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tessa Thompson akiwa San Diego Comic-Con Mwaka 2019

Tessa Lynne Thompson (alizaliwa Los Angeles[1], Kalifornia, Oktoba 3, 1983) ni mwigizaji wa filamu wa Marekani.

Alianza kazi yake ya kuigiza akiwa pamoja na kampuni ya wanawake ya Los Angeles ya Shakespeare akiwa anasoma katika Chuo cha Santa Monica, aliigiza kwenye filamu ya maonyesho kama The Tempest na Romeo na Juliet. Alipata mafanikio na umaarufu baada ya kuigiza kwenye filamu ya Mississippi Damned (2009) akiigiza kama Tina Mabry na kwenye filamu ya Tyler Perry's For Colored Girls (2010).

Thompson alipata umaarufu na kufahamika kupitia vichekesho vilivyojulikana kama Dear White People (2014), na aliigiza kama Diane Nash mwanaharakati wa haki za raia katika igizo la kihistoria la Ava DuVernay Selma (2014). Alipata pia umaarufu kwa kuigiza kama Bianca Taylor kwenye filamu ya Creed (2015) Creed II (2018) na Creed III (2023). Pia aliigiza kama Valkyrie katika filamu za Marvel Cinematic Universe, ikiwa ni pamoja na Thor: Ragnarok (2017) na Thor: Love and Thunder (2022), pamoja na kua mwigizaji mkuu katika filamu ya Men in Black: International (2019). Alipokea sifa katika filamu za kujitegemea alizoigiza ambazo zilikua kama Sorry to Bother You (2018), Annihilation (2018), Sylvie's Love (2020), and Passing (2021), na baadae aliteuliwa kuwania tuzo za Filamu za British Academy Film Award.

Maisha ya Awali na Elimu

[hariri | hariri chanzo]
Thompson katika tuzo za 46 za NAACP Image Awards mwaka 2014

Thompson alilelewa kati ya Los Angeles na Brooklyn, New York[2]. Baba yake ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo Marc Anthony Thompson, ni Afro-Panamanian[3] na mwanzilishi wa muziki Chocolate Genius. Mama yake ni nusu mmexico na mzungu[4]. Dada yake mdogo, Zsela ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo[5].

Thompson alisoma katika shule ya Santa Monica ambapo aliigiza kama Hermia katika filamu ya wanafunzi iliyoitwa A Midsummer Night's Dream na alisoma chuo cha Santa Monica college (SMC) ambapo alisoma anthropolojia ya kitamaduni. Akiwa Santa Monica college (SMC) alihudhuria mihadhara ya Lisa Wolpe wa Kampuni ya Wanawake ya Los Angeles ya Shakespeare (LAWSC)[6].

  1. "Tessa Thompson Actor, Singer | TVGuide.com". web.archive.org. 2016-09-08. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-09-08. Iliwekwa mnamo 2024-04-20. {{cite web}}: Cite has empty unknown parameter: |dead-url= (help)
  2. "noverbet เข้าสู่ระบบ เว็บไซต์สล็อตเครือใหญ่ ทดลองเล่นฟรีระบบลื่นไหล โปรโมชั่นเต็มระบบ". noverbet (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-04-20.
  3. https://www.essence.com/awards-events/red-carpet/black-women-hollywood/tessa-thompson-speech-mexican-mother-pride-blackness/
  4. https://www.yahoo.com/movies/tessa-thompson-selma-dear-white-people-106538108532.html
  5. Benor, Dalya (2019-04-26), "Zsela Sings Moody Ballads for the Fashion and Art Set", The New York Times (kwa American English), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2024-04-20
  6. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2024-04-20. {{cite web}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)