Teknolojia ya wazi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkutano wa Teknologia ya wazi uliofanyika NASA Goddard Space Flight Center mnamo machi 17, 2010

Teknolojia ya wazi ni njia ya kuandaa na kuendesha mkutano au makongamano ya siku kadhaa ambayo washiriki wake wamealikwa ili kuzingatia na kujadili kazi muhimu au dhumuni ya mada husika.

Tofauti na makongamano yaliyopangwa awali ambapo mzungumzaji na muda wake wa kuzungumza hupangwa miezi kadhaa awali, na kwa hivyo kupelekea mabadiliko mengi. Vyanzo vya teknolojia ya wazi huwapa washiriki uwezo wa kufanya maandalizi pindi wanapokuwa kwenye ukumbi wa hafla ya moja kwa moja.

Ajenda na ratiba ya mikutano hujulikana kidogo au kuto tambuliwa kabisa hadi watu wanapo wasili. Mpangilio wa wasemaji, mada na maeneo huandaliwa na watu wanaohudhuria, mara tu wanapofika. Kila mkutano unaotumia teknolojia ya wazi unapoisha hati ya muhtasari huundwa ikitoa muhtasari wa kile kilichofanywa na kisichofanywa.

Teknolojia ya wazi ilianzishwa na Harrison Owen mnamo mwaka 1980. Ilikuwa moja ya zana bora kumi za maendeleo ya shirika zilizotajwa kati ya 2004 na 2013[1].

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ilianzishwa na Harrison Owen, Askofu ambaye historia yake ya kitaaluma ilizingatia asili na kazi ya hekaya, matambiko na utamaduni. Katikati ya miaka ya 1960, aliacha chuo na kufanya kazi na mashirika mbalimbali ikiwa ni pamoja na vijiji vidogo vya Afrika Magharibi, mashirika makubwa na mashirika yasiyo ya kiserikali, mashirika ya kijamii ya mijini (ya Marekani na Afrika).

Sambamba na hayo, aligundua kwamba utafiti wake wa hadithi, mila na utamaduni ulikuwa unatumika moja kwa moja katika mifumo hii kijamii. Mnamo 1977, alianzisha kampuni ya ushauri ili kuchunguza utamaduni wa mashirika katika mabadiliko kama mtaalamu wa nadharia na mshauri.

Harrison aliitisha Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Mabadiliko ya Shirika kama mkutano wa kitamaduni. Baadaye, washiriki walimwambia sehemu bora zaidi ni mapumziko ya kahawa. Alipofanya tena teknolojia ya wazi ilikuwa njia yake ya kufanya mkutano wote kuwa kama mapumziko ya kahawa, akizingatia kaulimbiu kuu (kusudi, hadithi au swali) ambayo itaongoza samarati ya kujitawala ya kikundi.

Jaribio la Owen lilikuwa la mafanikio ya kutosha na kupelekea mkutano wa Usanifu wa Shirika kuendelea kwa zaidi ya miaka ishirini kwa muundo wa teknolojia ya wazi. Lakini baada ya muda mfupi wa matumizi ya teknolojia ya wazi, washiriki walianza kuitumia katika kazi zao wenyewe na kuripoti katika mafunzo yao. Tukio moja lililofanyika India lillilokua na kaulimbiu ya 'Biashara ya Biashara ni Kujifunza,' lilivuta tahadhari ya vyombo vya habari vya ndani ambavyo vilishtua gazeti la New York Times, ambalo baadaye liliandika hadithi zao kuhusu teknolojia ya wazi, mwaka 1988 na 1994[2]. Owen aliandika mwongozo mfupi wa mtumiaji ili kusaidia majaribio na mazoezi zaidi. Hatimaye, mwongozo mpanuzi ulichapishwa na Berrett-Koehler.

Katika miaka ya 1980, Owen alifahamika na makampuni mengi makubwa kuwa mmoja kati ya washauri wa zama mpya ambao mbinu zao zinaweza kuchochea ushiriki wa wafanyakazi na maslahi katika matatizo ya kampuni[3].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Enrique V. Abadesco Jr (2015-12-20). "An updated definition of organizational development". INQUIRER.net (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-07-15. 
  2. Deutsch, Claudia H. (1994-06-05), "Round-Table Meetings With No Agendas, No Tables", The New York Times (kwa en-US), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2023-07-15 
  3. Cook, Karen (1988-09-25), "SCENARIO FOR A NEW AGE", The New York Times (kwa en-US), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2023-07-15