Nenda kwa yaliyomo

Tapinarof

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tapinarof, inajulikana pia kama benvitimod na kuuzwa kwa jina la chapa Vtama, ni dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa kingamwili kushambulia seli za kawaida kimakosa unaosababisha mabaka manene kwenye ngozi au kichwani (plaque psoriasis).[1][2] Inatumika kwa kupaka kwenye ngozi.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuhisi mwasho kwenye mrija unaozunguka mzizi na ncha ya nywele, na ugonjwa wa ngozi . [1] Ni kiamsha kipokezi cha aryl hidrokaboni. [1]

Tapinarof iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2022.[1] Haikudhinishwa Ulaya wala Uingereza kufikia mwaka wa 2022.[3] Nchini Marekani, gramu 60 za krimu 1% iligharimu takriban USD 1,400 kufikia 2022.[4]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "Vtama- tapinarof cream". DailyMed. 23 Mei 2022. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Julai 2022. Iliwekwa mnamo 19 Juni 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Stein Gold, Linda; Rubenstein, David S.; Peist, Ken; Jain, Piyush; Tallman, Anna M. (Septemba 2021). "Tapinarof cream 1% once daily and benvitimod 1% twice daily are 2 distinct topical medications". Journal of the American Academy of Dermatology. 85 (3): e201–e202. doi:10.1016/j.jaad.2021.04.103.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Tapinarof". SPS - Specialist Pharmacy Service. 29 Agosti 2020. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Januari 2022. Iliwekwa mnamo 12 Desemba 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Vtama Prices, Coupons, Copay & Patient Assistance". Drugs.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 12 Desemba 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)