Tabora United
Kitayosce ni klabu ya soka yenye maskani yake mjini Tabora, wilaya kuu ya Mkoa wa Tabora nchini Tanzania . Kwa sasa inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Klabu ya soka ya Kilimanjaro Talented Youth Sports Center (Kitayosce) ilianzishwa Ruangwa, mojawapo ya wilaya sita za Mkoa wa Lindi . [1] Baadaye ilinunuliwa na mwenyekiti wa sasa, Yusuf Kitumbo huku ikishiriki Ligi ya Kwanza. Ilihamia Manispaa ya Tabora. Msimu wa 2018–19, walimaliza nafasi ya pili katika ligi daraja la pili chini ya uangalizi wa kocha msaidizi, Ally John Shangalu na kupandishwa kwenye michuano ya ligi daraja lwa kwanza kwa mara ya kwanza.
Mnamo 2023, baada ya kumaliza nafasi ya pili Ligi Daraja la kwanza, walipanda daraja hadi Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza. [2]
Benchi la Ufundi
[hariri | hariri chanzo]Wanafunzwa na Kefa Kisala, [3] kocha wa zamani wa Masaka LC FC, Express FC, URA FC, BUL FC, Wakiso Giants, UPDF FC [4] na kocha msaidizi The Cranes . [5]
Rangi na beji
[hariri | hariri chanzo]Rangi za Kitayosce ni bluu na nyeupe wakiwa nyumbani na kijani na nyeupe michezo ya ugenini. Beji ya Kitayosce FC ina kifupi kilichoandikwa karibu na picha ya Mlima Kilimanjaro, miale ya jua kwenye soka na jina kamili la klabu.
Uwanja
[hariri | hariri chanzo]Kitayosce wanacheza mechi zao za nyumbani kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora . [6]
Wafuasi
[hariri | hariri chanzo]Wanatoa mashabiki wao kutoka kwa wakazi 226,999 wa wilaya ya Tabora .
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Tanzania, World places. "Kilimanjaro Talented Youth Sports Centre - Kitayosce". tanzania.worldplaces.me. World places. Iliwekwa mnamo 7 Septemba 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Wathiongo, Ngugi (2023-06-05). "Timu Zilizofuzu Ligi Kuu NBC 2023/24". Ligi Kuu Tanzania (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-06-10.
- ↑ Kefa, Kisala (18 Julai 2022). "Reports: Kefa Kisala set to join Tanzanian second division club". ndibba.com. Saul Mata Tadeo. Iliwekwa mnamo 18 Julai 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kefa, Kisala (9 Julai 2018). "Kefa Kisala beats Bamweyana, Bisaso to Express F.C head coach job". kawowo.com. DAVID ISABIRYE. Iliwekwa mnamo 9 Julai 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Tanzania, Championship (18 Aprili 2022). "Ihefu, Kitayosce challenge DTB reign at helm". africa-press.net. Africa-Press – Tanzania. Iliwekwa mnamo 18 Aprili 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Ali Hassan, Mwinyi Stadium. "ALI HASSAN MWINYI STADIUM". Soccerway. Soccerway. Iliwekwa mnamo 1 Julai 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)