TaTEDO

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

TaTEDO[hariri | hariri chanzo]

TaTEDO ni Shirika la Kijasiriamali la Kitaifa, lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na uendelezaji wa nishati endelevu za kisasa. Shirika hili lina uzoefu wa kuendeleza nishati mbadala tangu 1990, katika utengenezaji wa sera za nishati, upangaji wa miradi na utafiti katika maeneo ya kufanyia kazi za miradi.

KUANZISHWA[hariri | hariri chanzo]

TaTEDO ilianzishwa tarehe 20 mwezi wa tano mwaka 1990.

MAKAO MAKUU[hariri | hariri chanzo]

Makao yake makuu yako Dar es salaam, Tanzania.

HISTORIA YA TaTEDO[hariri | hariri chanzo]

Mwanzo wa TaTEDO unaweza kwenda hadi miaka ya 1980 wakati mmoja wa waanzilishi wake (Nd. Estomih Sawe) alipopata nafasi ya kwenda nje ya nchi kwa masomo zaidi katika masuala ya nishati. Baada ya kurudi masomoni alifanya kazi katika Wizara ya Nishati, Madini na Maji ambapo alishiriki katika kuunda na kuendeleza kitengo cha nishati mbadala (au nishati za kujadidika). Katika miaka ya 1985 hadi 1989, alishiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali kama mradi wa nishati wa GTZ katika mikoa ya Dar es salaam, Mafia na Kondoa. Mradi mwingine ulikuwa wa majiko na uchomaji mkaa uliofadhiliwa na Benki ya Dunia ambao ulipitishwa mwaka 1988. Katika utekelezaji wa mradi huu, wataalamu kadhaa kutoka nje ya nchi waliajiriwa akiwemo Dk. Maxwell Kinyanjui kutoka Kenya (Mtaalam wa Majiko), Ibrahim Ndiaye kutoka Senegali (mtaalam wa uchomaji mkaa) na Rainer German (Mtaalam wa Tanuru la Nusu Chungwa). Kulikuwa na majadiliano ya mara kwa mara kati ya Nd. Sawe na Dk Kinyanjui ambayo yalikuwa yakiendelea hata baada ya saa za kazi . Kati ya changamoto ambazo walikutana nazo wataalamu hawa ilikuwa namna ya kuweza kukifanya haya yaliyoletwa na mradi mradi kuwa endelevu. Mawazo mbalimbali yalipendekezwa ikiwa ni pamoja na kuanzisha kiwanda cha uzalishaji wa majiko sanifu. Hata hivyo mawazo haya yalishindikana kutokana na kukosekana kwa wajasiriamali waliokuwa tayari kuwekeza katika biahara ya majiko sanifu Mwaka 1989, lilijitokeza wazo la kuanzishwa kwa taasisi isiyo ya kiserikali ya nishati katika majadiliano baina ya Mr Sawe na Dk Kinyanjui. Wazo hili lilikubaliwa na wataalam hawa wawili kwa kuzingatia mafanikio ya asasi nyingine kama KENGO ya Kenya.

Jina la Taasisi/Shirika[hariri | hariri chanzo]

Majadiliano yaliendelea ili kupata jina la asasi. Dk Kinyanjui alipendekeza jina la Tanzania Wood Energy Non-Governmental Organization (KWENGO). Jina hilo lilikubaliwa na katiba ya mwanzo iliandaliwa kwa kutumia jina hili. Baada ya muda Nd. Sawe aliona ni vizuri ikaanzishwa asasi ambayo itajumuisha teknolojia nyingine za kujadidika za nishatu na jina la asasi likabadilika kuwa “Tanzania Traditional Energy Organization”(TaTEDO)

Kumtambulisha Dakta Kinyanjui[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1989 Nd Sawe alimtambulisha Dk Kinyanjui kwa Mzee Daniel Yona na Mwalimu Joshua Meena ambaye kwa wakati huo alikuwa mwalimu Mstaafu na Mzee Yona alikuwa mfanyabiashara. Wote walikubaliana na wazo hilo na wakaanza mikutano ya pamoja ya kuanzisha TaTEDO.

Mkutano wa kwanza wa kuanzisha TaTEDO[hariri | hariri chanzo]

Mkutano wa kwanza ulifanyika nyumbani kwa Mzee Yona mwaka 1990 ambao uliongelea katiba ya kwanza walioudhuria walikuwa waanzilishi wa TaTEDO Mzee Daniel Yona, Mwalimu Joshua Meena , Nd. Estomih Sawe na Dk Maxwell Kinyanjui Katika kikao hiki katiba ya kwanza ya TaTEDO iliyoandaliwa na Bwana Sawe na Dakta Maxwell ilijadiliwa na kuamuliwa kusajili Asasi hii baada ya katiba kupitiwa na mwanasheria Bwana Temu. Iliamuliwa pia kuongeza watu wengine ili kufikia idadi ya watu kumi na mbili waliotakiwa kwa ajili ya usajili.

Mwenyekiti wa Kwanza wa TaTEDO[hariri | hariri chanzo]

Kikao cha kwanza cha taasisi kilimteua Mzee Yona Kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa TaTEDO, Mr. Estomih Sawe kuwa makamu wa mwenyekiti, Mwalim Meena katibu wa kwanza na Dr Maxwell alipendekezwa kuwa mshauri Waanzilishi hawa wane walichangia jumala ya Shilingi 52,000 kuwezesha usajili wa TaTEDO. mwenyekiti na katibu walipewa jukumu la kusajili taasisi KWA SABABU Bwana Sawe na Dakta Maxwell walikuwa bado wafanyakazi wa serikali.

Kuzaliwa TaTEDO[hariri | hariri chanzo]

Mwenyekiti na katibu walifuatilia usajili ambao ulitolewa tarehe 29/5/1990 na hii ndio siku rasmi ya kuzaliwa TaTEDO.

Awamu ya kwanza[hariri | hariri chanzo]

Awamu ya kwanza ya TaTEDO ilikumbwa na changamoto nyingi kutokana na uzoefu mdogo wa taasisi zisizo za kiserkiali wa wanzilishi wa taasisi. Awamu hii TaTEDO iliongozwa na Mwalimu Joshua Meena. Hata hivyo kwa ushiriakino na wadau mbalilmbali TaTEDO iliweza kusimama. Wanachama wa kwanza wa TaTEDO walikuwa ni mafundi wa majiko sanifu pamoja na wakulima. Katika kipindi hiki tatedo ilifanya kazi Dar es Salaam peke yake. Katika kipindi hiki TaTEDO ilipata Ufadhili Kutoka HIVOS mwaka 1992, NORAD mwaka 1993, FINNIDA, pamoja na CIDA.

Mabadiliko ya Uongozi[hariri | hariri chanzo]

Mabadiliko ya uongozi mwaka 1997 Mwaka 1996 mwalimu Meena aliomba kupumzika na hivyo kufikia mwisho wa awamu ya kwanza. TaTEDO iliamua kutafuta mtu mwenye utaalam wa Nishati Jadidifu ili kuongeza kasi ya maendeleo ya Tassisi. Uongozi mpya chini ya Mkurugenzi wa sasa Bwana Sawe uliingia ukiwa na mikakati mipya ya kuendeleza huduma za nishati endelevu. katika kipindi hiki dhamira na maono ya Tasisi yalibadilika ambapo

Mikakati ya Taasisi[hariri | hariri chanzo]

Taasisi ilianza mikakati ya kuboresha uwezo wa rasilimali watu kwa kuajiri wasomi na kuendeleza waliopo. Katika kipindi hiki taasisi imeongeza uwezo wa rasilimali watu. Na kuongeza eneo la utendaji kazi kutoka mkoa mmoja wa Dar es Salaam hadi mikoa mitano ya Arusha, Pwani, Kilimanjaro, Mwanza na Shinyanga.

Raslimali Watu[hariri | hariri chanzo]

Pia katika kipindi hiki idadi ya wafanyakazi imeongezeka kutoka 15 mwaka 1996 hadi 56 mwaka 2010.

Fedha Kuongezeka[hariri | hariri chanzo]

Katika kipindi cha miaka ishirini ya TaTEDO kiasi cha fedha kinachotumika kwa mwaka kimeogezeka kutoka shilingi 54,000 mwaka 1990 hadi shilingi billion 2.9 mwaka 2009.

Muundo wa Taasisi[hariri | hariri chanzo]

Muundo wa Taasisi ni kama ifuatavyo Mkutano Mkuu wa wanachama wote, Bodi ya Wakurugenzi, Mkurugenzi Mtendaji,

Teknolojia za TaTEDO[hariri | hariri chanzo]

Teknolojia za Nishati Mbadala ambazo zinaendeleshwa na TaTEDO kibiashara ni kama zifuatavyo

i)Majiko sanifu ambayo yanatumia kuni chache/kidogo ikilinganishwa na majiko ya mafiga matatu,
ii)Umeme wa nishati ya jua ambao umekuwa ni mkombozi kwa vituo vya afya vijijini na mashuleni
iii)Mtambo wa kuchajia simu ambao umekuwa ni kichocheo cha kuongeza kipato kwa wajasiriamali wa nishati mbadala vijijini,mtambo
    huu unatumika katika maeneo ya vijijini ambapo hamna grid ya Taifa
iv)Kaushio linalotumia mwanga wa jua kukaushia mazao ya vyakula na mboga mboga
v)Mtambo wa huduma anuwai za nishati(ESP/MFP) mtambo huu ambao unafungwa vijijini ili kuzalisha umeme maeneo ya vijijini
vi)Oven ya kuokea mikate na keki

Kupitia teknolojia za TaTEDO wajasiriamali zaidi ya 270 nchini Tanzania wameweza kujiongezea kipato na kuboresha mazingira

MIRADI YA TaTEDO[hariri | hariri chanzo]

MIKOA YA MIRADI[hariri | hariri chanzo]

WADAU WA MAENDELEO YAANI WAFADHILI[hariri | hariri chanzo]