Nenda kwa yaliyomo

Suzi Lovegrove

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Suzi Lovegrove (1955 - 1987) alikuwa raia wa Australia mzaliwa wa Marekani aliyekuwa na VVU.

Mnamo mwaka 1987 Hadithi ya Suzi, ilionyeshwa kwa mara ya kwanza kwenye runinga ya Australia. Troy ambaye ni mtoto wa Suzi aliambukizwa virusi tangu akiwa tumboni. Mnamo mwaka 1993 alifariki akiwa na umri wa miaka saba.

Hapo mwanzo Suzi Lovergrove alikuwa mwigizaji aliyejulikana kama Suzi Sidewinder. Mnamo mwaka 1983 Suzi alihusika katika sehemu ndogo ya filamu iliyojulikana kwa jina la Crazy, akicheza kama mshiriki wa bendi ya Nada, (Nada alicheza na rafiki wa Suzi aitwaye Lori Eastside ambaye baadaye alikuja kuonekana kidogo katika "Suzi's Story"). Walipokuwa kenye ndege wakitazama sinema kati ya Marekani na Australia, ni wakati ambapo Suzi alibahatika kukutana na mume wake wa baadaye aitwaye Vince Lovegrove. Miaka ya 1960 Vince alikuwa mwimbaji kiongozi wa The Valentines na kisha aliendelea kusimamia Divinyls na Jimmy Barnes[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Suzi Lovegrove kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.