Nenda kwa yaliyomo

Suzanne Lenglen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Suzanne Lenglen

Suzanne Lenglen (24 Mei 18994 Julai 1938) alikuwa mchezaji maarufu wa tenesi wa Ufaransa aliyeibuka na umaarufu katika miaka ya 1920 kwa kushinda michuano kadhaa, ikiwemo sita ya Wimbledon.

Alivunja vizuizi vya kijinsia katika michezo na alikuwa na mtindo wa pekee wa uchezaji. Alistaafu mwaka 1926[1].


Lenglen ameheshimiwa kwa njia mbalimbali katika Mashindano ya Ufaransa (French Open). Katika Stade Roland Garros, Uwanja wa Suzanne Lenglen, uwanja wa pili kwa ukubwa wa maonesho uliyojengwa mwaka 1994 ukiwa na uwezo wa kuketi watu wapatao elfu kumi, ulipewa jina lake mwaka 1997.[2][3] Nje ya uwanja huo, kuna sanamu ya ukumbusho wa shaba yenye umbo la Lenglen iliyowekwa mwaka 1994. Shirikisho la Tenisi la Ufaransa (FFLT) lilikuwa limepanga kuanzisha sanamu mara baada ya kifo chake, lakini mpango huo haukufanikiwa kutokana na kuanza kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwaka huo huo. Aidha, moja ya milango mikuu ya kuingia uwanjani inajulikana kama Porte Suzanne Lenglen, inayoelekea kwenye Allée Suzanne Lenglen. Vilevile, kombe la ubingwa wa wanawake la singles lilibatizwa jina la Coupe Suzanne Lenglen mwaka 1987. Pamoja na mafanikio yake katika Mashindano ya Ufaransa, Lenglen hakuwahi kushindana katika Stade Roland Garros kwa kuwa hayakuwa makao ya mashindano hadi mwaka 1928, baada ya yeye kustaafu kutoka tenisi ya ridhaa (amateur).[3]

Lenglen alijumuishwa kwenye Jumba la Heshima la Kimataifa la Tenisi (International Tennis Hall of Fame) mwaka 1978. Baada ya kifo chake, alipewa Nishani ya Heshima ya Taifa la Ufaransa (Cross of the Legion of Honour). Pia, barabara nyingine nje ya Klabu ya Tenisi ya Nice Lawn ilipewa jina la Avenue Suzanne Lenglen kwa heshima yake.[3] Amewahi pia kuheshimiwa na Google Doodle mara mbili, mara ya kwanza katika kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa ya 117 mnamo 24 Mei 2016, na mara ya pili katika Siku ya Wanawake Duniani mnamo 8 Machi 2017.[4][5]

  1. https://www.britannica.com/biography/Suzanne-Lenglen
  2. "Roland Garros". International Tennis Federation. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Novemba 2019. Iliwekwa mnamo 10 Novemba 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 1 2 3 Little 2007, p. 124.
  4. "Suzanne Lenglen's 117th Birthday". Google. Iliwekwa mnamo 10 Novemba 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "International Women's Day". Google. Iliwekwa mnamo 8 Machi 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Suzanne Lenglen kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.