Nenda kwa yaliyomo

Suleiman Abdullahi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Suleiman Abdullahi (alizaliwa Kaduna, Nigeria, 10 Disemba 1996) ni mwanasoka wa kulipwa kutoka Nigeria ambaye anacheza kama mshambuliaji katika klabu ya Allsvenskan IFK Göteborg.

Abdullahi alijiunga na klabu ya Viking FK mnamo mwaka wa 2015. Mnamo Juni 2016, Abdullahi alihamia klabu ya Eintracht Braunschweig katika ligi ya Ujerumani, Bundesliga kwa mkataba wa miaka minne. Katika misimu miwili aliyocheza katika klabu ya Braunschweig alicheza mechi 41 za ligi akifunga mabao 8 na kutengeneza asisti 6. [1]

Mnamo Agosti 2018, kufuatia Braunschweig kushuka daraja, Abdullahi alijiunga na klabu ya FC Union Berlin kwa mkopo na baada ya hapo mnamo tarehe 1 Juni 2019, FC Union Berlin ilimsajili Abdullahi kwa uhamisho wa kudumu.[2]

Hatimaye, mnamo tarehe 28 Juni 2022, Abdullahi alirejea katika klabu yake ya awali ya IFK Göteborg iliyopo nchini Uswidi na alitia saini mkataba utakaodumu hadi mwishoni mwa mwaka 2025.[3]

  1. "Union leiht Suleiman Abdullahi aus", kicker Online, 21 August 2018. Retrieved on 21 August 2018. (German) 
  2. "Rückkehr perfekt: Braunschweig holt Abdullahi zurück". kicker (kwa German). 16 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo 16 Agosti 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unrecognized language (link)
  3. "Suleiman är klar!" (kwa Kiswidi). Göteborg. 28 Juni 2022. Iliwekwa mnamo 22 Julai 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Suleiman Abdullahi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.