Nenda kwa yaliyomo

Steven Dese Mukwala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Steven Dese Mukwala[1] (alizaliwa 12 Julai 1999) ni mchezaji wa soka kutokea nchini Uganda.

Alianza kucheza katika timu ya vijana ya Kampala Junior Team (KJT) kabla ya kujiunga na Vipers SC[2]. Mwaka 2019, alicheza kwa mkopo katika klabu ya URA FC na kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Uganda kwa mabao 13. Baadaye, alienda St. George SC ya Ethiopia na Asante Kotoko ya Ghana. Mwaka 2024, alijiunga na Simba S.C.[3] kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufunga mabao. Mukwala pia ni mchezaji muhimu katika timu ya taifa ya Uganda, The Cranes.

  1. "Vipers SC yamsajili mshambuliaji kijana Mukwala Steven". 23 Juni 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-04-04. Iliwekwa mnamo 2024-08-06.
  2. "AFCON U23 Kufuzu: Kikosi cha Kobs cha wachezaji 23 chaitwa kwa kambi ya makazi". 11 Novemba 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-04-04. Iliwekwa mnamo 2024-08-06.
  3. https://www.habariforum.com/cv-ya-steven-mukwala-mchezaji-mpya-wa-simba-2024-2025/ Simba
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Steven Dese Mukwala kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.