Feleji isiopatadoa
Feleji isiopatadoa (kwa Kiingereza: stainless steel) ni aloi ya feleji yenye kiwango cha chromi ambayo ni kinga dhidi ya kutu inayosaidia kutoshika kutu haraka.[1] [2]
Ufafanuzi
[hariri | hariri chanzo]Feleji isiopatadoa haithiriwi na madoa, kutu, asidi na ulikaji kirahisi kama chuma au feleji ya kawaida. [3]
Tabia hii inapatikana kama aloi ya feleji ina kiwango cha angalau asilimia 11 za kromi, pia kiwango cha kaboni katika masi yake isizidi % 1.2.
Utendanaji wa kromi
[hariri | hariri chanzo]Ilhali feleji ya kawaida inatendana na maji na oksijeni kuunda kutu ambayo ni tabaka usoni isiyo imara inayoelekea kuachana na feleji na hivyo kuendelea kuipunguza, kromi inatendana na oksjeni kuunda tabaka jembamba sana ya oksidi ya chromi ambayo ni ngumu ilhali haiachani na feleji yenyewe. Hivyo inaunda tabaka imara inayozuia sehemu za feleji chini yake kuathiriwa.
Kuna aina tofautitofauti za feleji isiopatadoa; inawezekana kuunga madini mengine katika aloi; nyongeza za nikeli au molibdeni katika aloi zinaweza kuongeza uwezo wa kudumu katika mazingira penye asidi fulani au chumvi nyingi.
Namna ya kuongeza au kupunguza viungo katika aloi inabadilisha pia tabia nyingine kama uthabiti dhidi ya aina tofauti za shinikizo, ugumu, kiwango cha kuvunjika
Historia
[hariri | hariri chanzo]Feleji isiopatadoa ilianza kutambuliwa katika karne ya 19 lakini wakati ule teknolojia haikupatikana bado kwa uzalishaji wake; tangu mwanzo wa karne ya 20 ilianza kutengenezwa katika viwanda.
Uzalishaji wake duniani kote kwenye mwaka 2018 ulikuwa tani milioni 50.7[4]
Matumizi
[hariri | hariri chanzo]Feleji isiopatadoa ina faida nyingi hivyo matumizi yake yameenea sana.
- nyumbani visu, umma, vijiko, bakuli na bilula za maji hupatikana vilivyotengenezwa kwa feleji hii
- katika shughuli za tiba vifaa vya matabibu hutumia feleji hii kwa sababu vinaumu na vinaweza kusafishwa kwa joto kubwa (lazima kwa kuua viini) bila kulika.
- katika tasnia ya vyakula vyombo vya feleji isiyopatadoa ni muhimu, hasa pale ambako viowevu kama maziwa na vinywaji hushughulikiwa
- ni muhimu katika tasnia ya kutegeneza madawa ambako usafi wa vyombo na dawa ni muhimu mno, vivyo hivyo kwa jumla katika shughuli za kikemia.
Feleji hiyo haiwezi kutumiwa kwa shughuli zote kwa sababu inavunjika rahisi zaidi kuliko feleji ya kawaida pia haivumilii aina mbalimbali za shinikizo.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "The stainless steel family" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2011-07-21. Iliwekwa mnamo 2009-11-12.
- ↑ "Steel glossary". American Iron and Steel Institute (AISI). Iliwekwa mnamo Julai 30, 2006.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Why is stainless steel stainless?". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-01-26. Iliwekwa mnamo 2008-12-20..
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-05-06. Iliwekwa mnamo 2019-12-22.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Makala kuhusu feleji isopata doa Archived 6 Januari 2009 at the Wayback Machine., kwenye tovuti ya International Stainless Steel Forum
- Je! Ni nini chuma cha pua Archived 31 Januari 2020 at the Wayback Machine. na BSSA
- Euro Inox (Lango la lugha nyingi)
- Habari kamili juu ya chuma cha pua na Kituo cha Habari cha pua
- Habari kamili juu ya madini ya chuma cha pua na Chuo Kikuu cha Cambridge
- Mzunguko wa maisha ugharimu chuma cha pua Archived 11 Novemba 2006 at the Wayback Machine.
- Utangulizi wa chuma cha pua na KOSA
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Feleji isiopatadoa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |