Nati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Aina mbalimbali za nati

Nati (kutoka Kiingereza nut) ni kishikizo ambacho kimetengenezwa kwa kawaida kwa chuma au feleji. Ina uwazi wa duara ndani yake yenye hesi.

Hutumiwa kwa kukaza parafujo aina ya bolti na hesi yake sharti kulingana kabisa na hesi ya parafujo yake.

Nati nyingi huwa na pande sita na kukazwa kwa spana.

Kuna pia nati zenya ala zinazozungushwa kwa mkono.